2


SI LA KULIKOSA

Sunday, March 26, 2017

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Simu: +255-22-2112035/40
Nukushi: +255-2122617/2120486
Baruapepe: ps@moha.go.tz
9 Barabaraya Ohio
S.L.P. 9223
11483 DAR ES SALAAM
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. John Pombe Joseph Magufuli
amewapandisha Cheo Maafisa sita wa Uhamiaji kuwa Makamishna wa Uhamiaji
kuanzia tarehe 28 mwezi Februari mwaka 2017, Wakati huo huo amewateua kushika
nyadhifa mbalimbali katika Jeshi la Uhamiaji.
Walioteuliwa kushika nyadhifa hizo ni Mrakibu wa Uhamiaji (SI) Edward Peter Chogero
kuwa Kamishna wa Divisheni ya Fedha na Utawala, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji
(SSI) Samwel Rhobby Magweiga kuwa Kamishna wa Divisheni ya Udhibiti na Uongozi
wa Mipaka, Mrakibu Mwandamizi (SSI) wa Uhamiaji Gerald John Kihinga kuwa
Kamishna wa Divisheni ya Pasipoti na Uraia, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI)
Musanga Mbusuro Etimba kuwa Kamishna wa Divisheni ya Hati za Ukaazi na Pasi,
Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Hannerole Morgan Manyanga kuwa Kamishna
wa Divisheni ya Sheria.
Aidha Mh.Rais amemteua pia Naibu Kamishna wa Uhamiaji Mourice David Kitinusa
kuwa Kamishna Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA). Uteuzi huo unaanzia tarehe
28 mwezi Februari mwaka 2017.
Imetolewa na
Meja Jenerali Projest Rwegasira
Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
26 Machi 201
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu