NA MWANDISHI MAALU, BUZWAGI
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa(anayechota mchanga pichani), amefanya ziara kwenye mgodi wa
dhahabu wa Buzwagi uliopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga na kuchukua sampuli
za mchanga katika makontena mbalimbali kwa lengo la kwenda kuyapima kwa
wataalamu wa madini ili kubaini kiasi cha dhahabu kilichomo.
Amesema wanataka kuona mchanga unaosafirishwa na mwekezaji huyo
unakiasi gani cha dhahabu, pia Serikali inataka kufahamu kama kodi inayolipwa
ni sahihi.” Hata hivyo tayari Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli alishatoa
tangazo la kuzuia usafirishaji wa michanga kwenda nje ya nchi,”.
Waziri Mkuu alitembelea mgodi huo jana jioni (Jumatatu, Machi
27, 2017) na kuchukua sampuli za mchanga kwa lengo la kuondoa mashaka juu ya
kinachosafirishwa. Sampuli hizo amezichukuwa kwenye makontena yaliyofungwa kwa
ajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi.
“Tumeamua kuchukua sampuli za mchanga ambao mwekezaj anasema
wanaupeleka nje ya nchi kwa ajili ya kwenda kutenganisha madini ya dhahabu na
shaba. Hata hivyo nimemuhoji kwa nini mitambo hiyo isiletwe nchini ili kila
kitu kifanyike hapahapa,”
Waziri Mkuu amesema sera ya uwekezaji inasema mtambo huo
unatakiwa uwepo nchini ili kila hatua ya uchenjuaji ifanyike hapa hapa, hivyo
tunataka kujiridhisha na mwenendo wa mwekezaji na mapato tunayoyapata kama
yanastahili.
Aliongeza kwamba “Hili lipo miongoni mwa masharti ya uwekezaji
kwenye sekta ya madini nchini kwamba mitambo hiyo ije kujengwa hapa nchini na
itaongeza fursa ya ajira na kukuza sekta nyingine ikiwemo ya kilimo,”.
Wakati huohuo Waziri Mkuu amewataka Watanzania kuwa nasubira
wakati Serikali ikiendelea na zoezi la kuchunguza athari zitokanazo na
kusafirisha mchanga wa madini nje ya nchi. Pia amewatoa wasiwasi
wafanyakazi katika migodi na wamiliki kutowapunguza na badala yake waache
waendelee na majukumu yao.
Kwa upande wake Meneja Uendelezaji wa mgodi huo Bw. George
Mkanza alisema mgodi huo ulionzishwa mwaka 2009 umeajiri watumishi 720 pamoja
na vibarua 500.
Alisema kwa siku wanachenjua makontena matatu hadi sita ambapo
katika kila kontena moja wanapata kilo tatu za madini ya dhahabu na tani nne za
madini ya shaba.
Bw. Mkanza alisema wanazalisha asilimia 50 ya madini ya dhahabu
na asilimia 50 ya dhahabu iko kwenye mchanga na inakuwa imechanganyika na
madini ya shaba ambayo ndiyo unaosafirishwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya
kutenganishwa.
“Hapa Buzwagi tuna makontena 179, makontena mengine 152 yako Dar
es Salaam kwenye bandari kavu ya Nazam na 21 yako bandarini. Kila siku
tunapoendelea kuzalisha tunakuwa na makontena manne hadi sita. Ndugu zetu wa
Bulyanhulu nao wanamakontena 108 yako mgodini na 104 yako Nazam Cargo Dar es
Salaam,” alisema.
Mtaalamu
wa Madini akiweka Sampuli ya Mchanga katika Mfuko kutoka katika baadhi ya
Makontena na kumkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa nakuondoka nao kwa ajili ya
kuupeleka katika Maabara ya Serekali inayo shugulika na Upimaji wa Madini Wziri
Mkuu alifanya ziara katika mgodi wa Buzwagi 27March2017 kwalengo ya kujionea
aina ya Mchanga unao safirishwa nnje ya Nnchi na Baadhi ya Migodi inayo Chimba
Dhahabu hapa Nchini
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa afanya ziara katika Mgodi wa Buzwagi 27 March 2017 kwa ajili ya kuangalia Mchanga
uliowekwa katika Makontena kwa ajili yakusafirishwa nje ya nchi katikati
ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi.
Zainabu Telaki, na kushoto ni Meneja
Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi
Bwana Stewart Hamilton (PICHA NA PMO)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu
wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro katika Uwanja wa Ndege wa Mgodi
wa Buzwagi 27March2017 katikati ni Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telaki Viongozi hao walifika kumpokea Waziri
Mkuu alipofika kuangalia shughuli za Mgodi wa Buzwagi uliopo wilaya Kahama Mkoa
wa Shinyanga.
Baadhi ya viongozi wa kampuni ya Acacia,
wakimsubiri Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye mgodi wa Buzwagi ulioko
Wilayani Kahama mkoani Shinyanga
0 comments:
Post a Comment