Wednesday, April 5, 2017

MAKAMU WA RAIS ALIPOWAKARIBISHA SERENGETI BOYS NYUMBANI KWAKE

1 2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys  jijini Dar es Salaam alipowaalika  nyumbani kwake na kupata nao chakula cha jioni kabla ya vijana hao kuondoka Tanzania..kuelekea katika michuano ya mataifa ya Afrika ya vijana chini ya umri wa miaka 17 itakayofanyika Gabon, Serengeti Boys wanaondoka  Aprili 5 kuelekea Morocco kuweka kambi ya maandalizi ya michuano hiyo.
3
Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Dr Harrison Mwakyembe akizungumza na kuwatakia vijana hao ambao wanakwenda kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya mataifa ya Afrika ya vijana chini ya umri wa miaka 17 itakayofanyika Gabon.
 Mjumbe wa Kamati ya uhamasishaji ya  vijana wa timu ya Taifa  ya mpira wa miguu chini ya miaka kumi na Saba “Serengeti Boys” Bibi Beatrice Singano akitoa maelezo mafupi jinsi kamati hiyo inavyofanya kazi ya kuhamasisha uchangiaji wa timu hiyo ) katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan jana Jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Selestine Mwesigwa (wa kwanza kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan kwa timu ya Serengeti Boys , kulia ni kapteni wa timu hiyo Bw. Issa Makame.
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Zanzibar Rashidi Ally Juma akitoa neno kwa vijana “Serengeti Boys”(hawapo pichani) katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan (wa kwanza kushoto) iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
6
Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys.
7 8 9 10
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys ambao wanakwenda kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya mataifa ya Afrika ya vijana chini ya umri wa miaka 17 itakayofanyika Gabon.

( PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-MTAZAMONEWS.COM )

+255 684 07 4444
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu