Friday, May 5, 2017

WAZIRI MWIGULU AWATAKA WASAIDIZI WAKE KUSIMAMIA HAKI ZA WAFANYAKAZI, PAMOJA NA KUONDOA URASIMU, AFUNGUA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA WIZARA YAKE KUJADILI UTEKELEZAJI WA BAJETI 2017/2018




Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati waliokaa), Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya (wa pili kushoto), Kamishna Jenerali wa
Jeshi la Magereza (CGP), Dk. Juma Malewa (kulia), Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi
wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, William
Mkombozi (kushoto), Katibu wa Baraza hilo, Amani Mashaka wakiwa katika picha ya pamoja
na Wajumbe wa Baraza hilo, mara baada ya Waziri Mwigulu kufungua Kikao cha Baraza hilo,
kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo.
Katika hotuba yake, Mwigulu aliwataka wafanyakazi wa Wizara yake kuwa wavumilivu wakati
mahaitaji yao yanapofanyiwa kazi na viongozi wao, pia aliwataka watendaji wa wizara hiyo
kusimamia haki za wafanyakazi pamoja na kuondoa urasimu wa aina yoyote ili kuwaletea morali
ya kufanya kazi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.



Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto), akimsikiliza
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya mara baada ya Waziri Mwigulu
kufungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Mwigulu
aliwataka wafanyakazi wa Wizara yake kuwa wavumilivu wakati mahitaji yao yanapofanyiwa
kazi na viongozi wao, pia aliwataka Watendaji wa Wizara hiyo kusimamia haki za Wafanyakazi
pamoja na kuondoa urasimu wa aina yoyote ili kuwaletea morali ya kufanya kazi. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nch

Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na wajumbe
wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara yake kabla ya kufungua Kikao Baraza hilo kilichojadili
Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2016/2017 na malengo ya mwaka 2017/2018, kilichofanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake,
Mwigulu aliwataka Wafanyakazi wa Wizara yake kuwa wavumilivu wakati mahitaji yao
yanapofanyiwa kazi na viongozi wao, pia aliwataka watendaji wa wizara hiyo kusimamia haki za
wafanyakazi pamoja na kuondoa urasimu wa aina yoyote ili kuwaletea morali ya kufanya kazi.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa
akizungumza katika Kikao kilichojadili Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2016/2017 na malengo
ya mwaka 2017/2018 cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo kilichofanyika katika Ukumbi
wa Mikutano wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Naibu Inspekta Jenera
wa Polisi, Abdulrahman Kaniki na kulia ni Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la
Magereza, Gaston Sanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu