NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar , Abdulla Juma
Saadalla “ Mabodi” amesema CCM
itaendelea kufanya ushindani wa sera za maendeleo zitakazowanufaisha wananchi
wa makundi yote mijini na vijijini.
Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua Mafunzo ya
Wanawake na Uongozi kwa wanachama na viongozi wa UWT Mkoa wa Mjini huko Amani
Zanzibar, Dkt. Mabodi alisema wananchi
wa visiwa vya Zanzibar kwa sasa wanachohitaji ni siasa za ushindani wa kisera
katika kukuza kipato cha mwananchi mmoja
mmoja hadi taifa kwa ujumla.
Dkt. Mabodi alisema taifa lolote linalotamani
kuendelea kiuchumi ni lazima wananchi wake wakubali kwa vitendo dhana ya siasa
za ustaarabu katika kudumisha amani na utulivu wa nchi ili kufanya kazi za
kujiongezea kipato na kukuza uchumi wa nchi.
Aidha Naibu
Katibu Mkuu huyo alisema ushindi wa CCM katika chaguzi mbali mbali za dola unatokana
na nguvu za Wanawake wa UWT katika
kuunga mkono harakati mbali mbali za kisiasa hadi kuhakikisha chama kinaingia
madarakani.
“ kila mtu ndani ya Chama Chetu anajua na kutambua
mchango wa Wanawake katika medali za kisiasa, wao ndio wamekuwa mstari wa mbele
kwa kila kitu ikiwemo kujitokeza kwa wingi kupiga kura halali za kuiletea
ushindi CCM.
Pia nakuahidini kwamba nitaendelea kuwa nanyi bega kwa
bega kwa lengo la kuimarisha chama na jumuiza zake sambamba na kuwaletea
wananchi maendeleo ya kudumu.”, alisema Dkt. Mabodi.
Kupitia
Mkutano huo Dkt. Mabodi aliwasihi viongozi na
watendaji wa Umoja wa Wanawake
Tanzania kushuka ngazi za chini za
uongozi hasa matawi na mashina kwa lengo la kuratibu changamoto
zinazowakabili wananchi ili zitafutiwe ufumbuzi wa kudumu na serikali.
Aliwapongeza
viongozi wa UWT waliojitolea kuanzisha mafunzo ya uongozi kwa wanawake wenzao
ili wapate ujuzi wa kufanya siasa za maendeleo zitakazowajengea ujasiri wa
kujenga hoja imara zinazokubalika katika ulimwengu wa siasa za ushindani.
Sambamba na hayo alimpongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa
Zanzibar Dkt. John Pombe Magufuli kwa
juhudi zake za kulinda rasilimali za nchi hasa kuthibiti mianya ya usafirishaji
wa Mchanga wa Madini unaosababisha upotevu wa fedha nyingi za umma.
Akizungumzia Uchaguzi wa ngazi ya Wadi unaoendelea hivi
sasa katika Chama na Jumuiya aliagiza kwamba kamati zinazosimamia zoezi hilo
zifanye kazi ya ziada ya kuhakikisha wanapatikana viongozi safi wasiokuwa na
sifa za usaliti.
Mapema akizungumza katika Mkutano huo Mwenyekiti wa
UWT Mkoa wa Mjini, Bi. Waridi Juma
Othman aliahidi kuwa wanawake hao watatumia vizuri mafunzo ya uongozi katika
siasa kama muongozo wa kufanya kazi za kisiasa kwa ufanisi mkubwa.
Akitoa neno la shukrani Mbunge wa Viti Maalum wanawake( MNEC),
Khadija Hassan Aboud alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wanawake
wa CCM ili waweze kuzitumika vizuri fursa za uongozi zinazopatikana ndani ya
chama na serikali kwa ujumla.
Mafunzo hayo ya siku moja yameandaliwa na Mbunge wa Viti Maalum
wanawake( MNEC), Khadija Hassan Aboud kwa kushirikiana na Mbunge wa Viti Maalum
Mkoa wa Mjini, Faharia Shomari Shomari Khamis.
0 comments:
Post a Comment