NA IS-HAKA
OMAR, ZANZIBAR.
UMOJA wa
Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) umewataka wanawake
kuchangamkia fursa za Uongozi wa ngazi mbali mbali kupitia uchaguzi
unaondelea hivi sasa ndani ya Chama na jumuiya zake.
Wito huo
umetolewa Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja huo Zanzibar Bi.Tunu Juma Kondo katika mwendelezo wa ziara ya
UWT ya kuzungumza na Viongozi wapya wa ngazi za matawi wa umoja huo uko
Jimbo la Kijini Wilaya ya Kaskazini
"A" kichama Unguja.
Awambia Akina Mama hao kuwa Uchaguzi wa ngazi mbali mbali unaoendelea katika taasisi hiyo ndio fursa moja wapo ya
wanawake kupata nafasi za uongozi ili
waweze kufikia malengo ya kupata uwakilishi wa viongozi wenye idadi sawa na
wanaume ndani ya Chama hicho.
Alifafanua
kuwa wanawake wanatakiwa kuondokana na dhana ya kuendelea kuongozwa kwa
kila nafasi za uongozi ndani ya CCM bali wanatakiwa kujiongeza kwa kuwania
wenyewe uongozi ndani ya chama hicho ili kuleta maendeleo endelevu ndani ya
chama na jumuiya zake.
Pia
alisisitiza viongozi hao kuwa pamoja na majukumu ya kiuongozi waliyonayo ni
lazima wawahamasishe kwa wingi wanawake kuwania nafasi za uongozi
ili kupata viongozi makini na wenye uwezo wa kwenda na kasi
za kiutendaji za chama hicho.
"Wanawake
wenzangu tutumieni fursa ya Uchaguzi wa Chama kuwania nafasi mbali mbali za
uongozi , tusisubiri nafasi za uteuzi bali tusimame wenyewe
kupambana kwa kuhakikisha nasi tunakuwa na nyadhifa za uongozi kama walivyo
wanaume kwani tunaweza wenyewe bila ya kuwezeshwa’’,. Alisema Bi.Tunu.
Akizungumza katika ziara hiyo Katibu
Msaidizi Idara ya Organazesheni UWT Zanzibar, Bi. Mgeni Ottow Alisema CCM atadumu
madarakani endapo viongozi mbali mbali wanaopatikana kupitia uchaguzi wa chama
hicho watakuwa na uzalendo wa kweli katika kulinda maslahi ya taasisi hiyo kwa
vitendo.
Bi. Mgeni
aliwasihi Akina Mama wa Umoja huo
kuhakikisha wanachagua viongozi waadilifu na wenye uwezo wa kubuni fursa mbali
mbali za maendeleo zitakazowanufaisha wanawake wenzao na chama kwa ujumla.
“ Wanawake ndio tegemeo la Chama chetu na
jumuiya kwa ujumla hivyo lazima tuwe wa kwanza kujitokeza kwa kila tukio
linalohusu uimarishaji wa chama chetu hasa michakato ya uchaguzi na tukiwa
wengi katika nafasi za uongozi ndipo tutakapopata nguvu za pamoja kutetea haki
zetu na kupinga kisheria udhalilishaji wa Wanawake”,. Aliseleza Bi. Mgeni.
Kwa Upande
wake Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kaskazini Unguja, Bi. Miza Ali Kombo amesema
zoezi la Uchaguzi kwa ngazi ya Wadi linaendelea vizuri kwani wagombea tayari
wamejaza fomu na kinachosubiriwa kwa sasa ni upigaji wa kura ili kupata
viongozi watakaoongoza ngazi hiyo kwa miaka mitano.
Naye Katibu
wa UWT Tawi la Muange, Bi. Waja Mnadhani Ali alieleza maratajio yake
baada ya kupata nafasi hiyo atafanya kazi za jumuiya na chama kwa umakini na
uadilifu ili kuwawakilisha vyema wanawake waliomuamini na kumpa ridhaa ya
uongozi huo..
MWISHO
Kaimu Naibu Mkuu wa UWT Zanzibar, Bi. Tunu Juma Kondo akizungumza na viongozi wa Matawi ya Jimbo Kijini Wilaya ya Kaskazini “A” kichama Unguja.Katibu Msaidizi wa Idara ya Organazesheni UWT Zanzibar, Bi. Mgeni Ottow akitoa nasaha kwa viongozi wa Matawi ya Jimbo Kijini Wilaya ya Kaskazini “A” kichama Unguja
Baadhi ya viongozi wa UWT wa Matawi jimbo la kijini Wilaya ya Kaskazini “A” kichama Unguja wakisikiliza kwa makini nasaha zinazotolewa na viongozi wa UWT Zanzibar uko Tawi la CCM Muange. |
0 comments:
Post a Comment