Saturday, August 5, 2017

 Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), wanawakaribisha wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam na Watanzania wote kwa ujumla, kushiriki kwenye maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani yanayotarajiwa kufanyika leo asubuhi 

Ambayo Kitaifa huadhimishwa tarehe 5, Mei ya kila mwaka, TAMA Tawi la Muhimbili imepanga kuadhimisha siku ya 4 Agosti, 2017, ambayo ni wiki ya unyonyeshaji.

Chama kinapenda kuwajulisha katika maadhimisho hayo, Chama  kitatoa huduma za upimaji wa Afya kwa wananchi bure kuanzia saa 2, asubuhi mpaka saa 11.00 jioni katika eneo la maegesho ya magari (OPD) karibu na lango kuu la kutokea nje ya Hospitali hiyo.

Huduma zitakazo tolewa ni pamoja na: 

a. Upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi na matiti

b. Upimaji wa shinikizola damu, sukari, uzito na urefu

c. Upimaji wa virusi vya ukimwi (VVU) kwa hiari

d. Ushauri kuhusu lishe bora 

e. Ushauri kuhusu uzazi wa mpango

f. Elimu juu ya unyonyeshaji sahihi kwa watoto chini ya umuri wa miaka mwili

g. Elimu juu ya afya ya kinywa na meno 

Aidha TAMA Muhimbili itakuwa na kongamano la Kisyansi la wakunga tarehe 7, Agosti 2017 saa tatu asubuhi katika ukumbi wa namba 60 uliyopo eneo la jengo la OPD ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi, Ukunga na Mazingira ya ndani ya Hospitali hiyo,  Agnes Mtawa.

Maadhimisho ya siku ya mkunga duniani mwaka huu wa 2017, yanabebwa na kauli mbiu isemayo " WAKUNGA, WANAWAKEN FAMILIA NI WASHIRIKA WA KUDUMU"  

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu