Thursday, December 14, 2017

TIMU YA STAND UNITED WAPATA MDHAMINI BIKO

 Mwakilishi toka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Kabora Mboya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi shilingi milioni moja kwa timu ya Stand United ikiwa ni sehemu ya udhamini toka Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya BIKO.
.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye suti) akimkabidhi jezi Mwenyekiti wa Klabu ya Stand United Charles Lugeta ikiwa ni sehemu ya ya udhamini toka Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya BIKO.

  Mbunge wa Shinyanga Mjini Steven Masele akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi shilingi milioni moja kwa timu ya Stand United ikiwa ni sehemu ya udhamini toka Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya BIKO.
Picha na Eliphace Marwa - Maelezo
  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Wilfred Kidau akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi shilingi milioni moja kwa timu ya Stand United ikiwa ni sehemu ya udhamini toka Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya BIKO.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wa tatu toka kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni mia moja Mwenyekiti wa Klabu ya Stand United Charles Lugeta ikiwa ni sehemu  ya udhamini toka Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya BIKO.
.
Na Anitha Jonas – WHUSM
13/12/2017
Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe  amewataka wachezaji wa Timu ya Stand United  kuchukua Kombe la Ligi Kuu .
Mheshimiwa Mwakyembe ametoa kauli hiyo alipokuwa katika mkutano wa kutangazwa kwa mdhamini wa timu hiyo ambaye ni BIKOSPORTS  aliyetoa udhamini wa Sh. Milioni Mia Moja pamoja na kununua jezi za wachezaji watakazo tumia katika msimu huu wa ligi.
“Soka la leo siyo kama la zamani linahitaji uwekezaji na pesa za kutosha kusaidia  kupata wachezaji wazuri wenye viwango vya juu,Makocha wenye uweledi  na mazingira mazuri ya kufanyia mazoezi kwa wachezaji,”Mhe.Dkt. Mwakyembe.
Naye Mweyekiti wa Timu ya Stand United Bw.Dkt. Ellyson Maeja alitoa shukrani kwa Kampuni ya Biko kwa udhamini huo na kuaahidi kutumia fedha hizo vizuri kwa manufaa ya timu ikiwa ni pamoja  kulipa mishahara ya wachezaji.
“Tunashukuru sana Biko kwa udhamini huu pia napenda kuwa hahikisha kuwa fedha hizi zitatumika vizuri pamoja na kuongeza chachu katika maendeleo ya timu ikiwemo kujituma kwa wachezaji wa timu na kuleta mafanikio makubwa katika msimu huu wa ligi,”Dkt.Mgeta.
Pamoja na hayo naye Mkurugenzi Mtendaji wa BIKO Bw.Charles  Mgeta alitoa wito kwa makampuni mbalimbali kujitokeza na kusaidia sekta ya michezo nchini kwa maendeleo ya taifa letu pia amewataka watanzania kuendelea kucheza bahati nasibu ya BIKOSPORTS sababu ni rahisi na unalipwa  kwa haraka.

                            *****************MWISHO*********************

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu