:Kaimu Rais wa Klabu ya Michezo ya Simba Bw. Salim Abdallah akieleza waandishi habari (hawapo pichani) kuwa msimamo wa serikali wameuelewa na watakwenda kuzungumza na mwekezaji wao Mohamed Dewji kuhusu kumpunguzia 1% na kumpa 49% badala ya 50% waliyokuwa wametangaza hivi karibuni kumpa jana jijini Dar es Salaam,pembeni yake ni Mwanasheria wa Klabu ya Michezo ya Simba Bw.Evodius Mtawala.
Serikali
yatoa Msimamo wake kwa Klabu ya Simba kuhusu suala la uwekezaji
Na Anitha Jonas –
WHUS
Serikali imetoa msisitizo
kwa Klabu ya Mchezo ya Simba kuzingatia sheria na kanuni zinayosimamia suala la
uwekezaji kwa Klabu zilizoanzishwa na wanachama ambapo wanachama wanachukua 51%
na mwekezaji anachukua 49%.
Msisitizo huo umetolewa
leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Dkt.Harrison Mwakyembe alipokutana na uongozi wa Klabu ya Simba na kuzungumza
nao kufuatia kutoa asilimia 50% kwa mwekezaji wa klabu hiyo Bw.Mohamed Dewji
waliyemtanganza hivi karibuni ambapo ni kinyume na sheria.
“Kanuni zinazosimamia
masuala ya udhamini kwa vilabu zilifanyiwa marekebisho Novemba 2017 kwa ambapo ilioneka ni vyema klabu za
michezo zilizoanzishwa na wanachama wanapopata muwekezaji basi mwekezaji
achukue 49% na wanachama kutoka na mchango wao kwa mkubwa kwa klabu hiyo basi
wapewe 51% lengo ikiwa ni mwanachama aweze kunufaika vizuri,”Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea kuzungumza
katika mkutano huo na waandishi wa habari Mheshimiwa Mwakyembe alisema kuwa serikali
ya awamu ya tano hajaja kuuwa michezo bali lengo lake ni kuboresha michezo na
kuifanya kuwa na tija zaidi pamoja na kuleta maendeleo endelevu katika sekta
hiyo.
Naye Katibu wa Baraza
la Michezo Taifa Bw.Mohamed Kiganga alieleza kuwa ofisi yake ipo katika
maandalizi ya kuwaandikia barua Klabu ya Simba ya wapamsisitizo wa Serikali
katika kuzingatia sheria katika suala la udhamini na barua hiyo itawafikia wiki
ijayo.
Kwa Upande wa Kaimu
Rais wa Klabu ya Simba Bw.Salim Abdallah alieleza vyombo vya habari kuwa
wanashukuru serikali kwa kuwaeleza kuwa milango iko wazi pale watakapo kuwa na
tatizo au watakapo hitaji ushauri wanaweza kuonana na watendaji wake.
**********Mwisho****
************MWISHO*********** |
0 comments:
Post a Comment