Wednesday, February 21, 2018

ACT KUJENGA SKIMU YA MAJI

NA MWANDISHI WETU KIBAHA.

ZAIDI ya wakazi 300 wa Kata ya Mbwawa wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani wanatarajiwa kunufaika na mpango wa uendelezaji wa zaidi hecta 300 za bonde la mto Ruvu kutokana na ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji.
Akizungumza mara baada ya kusomewa Taarifa ya Kata ya Mipango ya Maendeleo na diwani wa chama hicho kwenye kata hiyo, Ramadhan Kombo Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe alisema, chama chake kitaandaa mradi maalum wa skimu ya umwagiliaji kwenye bonde hilo.
Awali kwenye taarifa yake diwani huyo mbali ya kueleza miradi tisa iliyobuniwa kwenye kata yake alieleza changamoto ya ukosefu wa miundombinu ya umwagiliaji licha ya kuwa na bonde kubwa la kilimo cha mpunga.
Kwa mujibu Ofisa Kilimo  na Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Kata hiyo, Francis Paul kata hiyo ina zaidi ya Hekta 300 zinazofaa kuendesha kilimo cha umwagiliaji kwenye bonde la mto Ruvu.
Akifafanua namna mradi huo wa Skimu ya maji utakavyobuniwa na kupatikana, Zitto alisema chama chake kupitia Taasisi ya Wazalendo Foundations itaandaa mradi (andiko maalum) kwaajili ya kupeleka kwa wafadhili watakao jenga mradihuo.
"Hili jambo ni rahisi sana kwetu kwakuwa chama chetu kiko tofauti sana na vyama vingine, sisi sera zetu ni za siasa za maendeleo ya wananchi hatufanyi siasa za kuzungumzia watu na matusi" alisema.
"Ili tuweze kufanikiwa haraka kwenye suala hili wananchi lazima tuungane na kuanzisha chama cha wakulima wa mpunga au umoja wa wakulima wa mpunga haraka sana, kwani hakuna mfadhili atakae toa fedha zake kwa mtu mmoja mmoja," alieleza.
Viongozi wa Chama hicho wako kwenye ziara za kuhamasisha na kuchangia juhudi za maendeleo kwenye kata zinazoongozwa na madiwani wake kwenye mikoa yote ilikochaguliwa.
Chama hicho kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 kilifanikiwa kupata madiwani 43 ambapo hadi sasa kina madiwani 42 baada ya diwani wake mmoja kutangulia mbele za haki.
Katika kata hiyo viongozi wa chama hicho walitembelea miradi mbalimbali ukiwamo mradi wa wa jengo la darasa katika Shule ya Sekondari ya Mbwawa Miswe, Mradi wa Ujenzi wa choo cha darasa la Chekechea.
Katika hatua nyingine kata hiyo yenye wakazi zaidi ya 5500 walieleza kusikitika kwao kutokana na kero ya upatikanaji wa maji ya safi ya matumizi licha ya kuwapo kwa mitambo ya maji ruvu na hata miundombinu ya kusambaza maji kwenye kata yao kwa zaidi ya miaka sita.
Wananch hao walifikisha kilio hicho kwa Kiongozi huyo ambaye alilazimika kuchukua hatua za haraka ili wenye mamlaka nao wachukue hatua za hara na kufanikiwa kuapata majibu ya matumaini.
"Suala lenu la maji nimefanya juhudi hapahapa kwa kuwasiliana na watu wa Wizara ya Maji, na wao wamewasiliana wenyewe na wamesema kesho wanatuma watu kuja kuangalia tatizo ni nini.
MWISHO:

 Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe(kulia) akimsikiliza Diwani wa Chama hicho Kata ya Mbwawa mkoani Pwani, Ramadhan Kombo walipokwenda kukagua mradi wa darasa katika Shule ya Sekondari Mbwawa Miswe.

 Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe(kulia) akimsikiliza Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mbwawa Miswe,Halima Chawabwe Kibaha mkoani Pwani jana alipofika Shuleni hapo kukagua jengo la darasa. Kata hiyo inaongozwa na diwani wa Chama hicho.
 Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe (kulia),akizungumza na wanafunzi  Shule ya Sekondari Mbwawa Miswe Kibaha mkoani Pwani jana, alopokwenda kuangalia mradi wa darasa jipya.Kata hiyo inaongozwa na diwani wa chama hicho,Ramadhan Kombo.

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu