Saturday, March 17, 2018

SERIKALI YATOA HATI ZA KIMILA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - UTUMISHI na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Lunguya  wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa yenye lengo la kukagua maendeleo ya miradi  inayotekelezwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.


Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakipunga mikono kuwasalimu wananchi wa kijiji cha Lunguya  wilayani Kahama wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo yenye lengo la kukagua maendeleo ya miradi.
Mratibu wa MKURABITA Bi. Seraphia Mgembe (katikati ya umati) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Lunguya wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa yenye lengo la kukagua maendeleo ya mradi ya MKURABITA.

Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Lunguya  wilayani Kahama wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Jason Rweikiza (Mb) wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo yenye lengo la kukagua maendeleo ya miradi.

Mmoja wa wanufaika wa Hati ya Hakimiliki ya Kimila wilayani Kahama akitoa shukrani kwa Serikali kwa kitendo cha kutoa Hati za Hakimiliki za Kimila 275 kwa wananchi wa vijiji vya Lunguya na Segese.A

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu