Saturday, March 17, 2018

MAKAMU WA RAIS AFANIKISHA UCHANGIAJI UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA Yahoo/Inbox

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya uchangiaji wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Muheza iliyofanyika jana usiku katika hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana aliwezesha kupatikana kwa shilingi bilioni moja na milioni mia saba kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza.
Katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais aliwapongeza uongozi wa Wilaya ya Muheza na mkoa wa Tanga pamoja na wananchi kwa kuamua kujenga hospitali yao ya wilaya ili kuboresha hali ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Makamu wa Rais alisema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuimarisha ubora wa huduma za afya ikiwa ni pamoja na kupunguza idadi ya vifo vya watoto kutoka kiwango cha vifo 66 kati ya vizazi hai 1,000 hadi kufikia kiwango cha angalau vifo 40 kati ya vizazi hai 1,000. Aidha, Serikali imedhamiria kupunguza vifo vya wanawake wajawazito kutoka 556 kwa mwaka 2017 katika vizazi hai 100,000 hadi kufikia 292 ifikapo mwaka 2020.
Sambamba na hilo Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo tuna mkakati wa kujenga, kukarabati na kupanua miundombinu ya Vituo vya afya 208 ili kuimarisha utolewaji wa huduma mbalimbali za afya.
Makamu wa Rais ameutaka Uongozi wa mkoa pamoja na wa Wilaya ya Muheza kuupa kipaumbele mradi huu wa ujenzi wa hospitali ya wilaya na kuhakikisha wanaweka mradi huu katika bajeti zinazokuja pamoja na kutafuta wahisani wengine wa ndani na nje ya nchi ili kuwezesha ujenzi wa hospitali hiyo kukamilika kwa haraka.
Makamu wa Rais aliwashukuru Wadau wote walioshiriki na kuomba kila mmoja wetu achangie kwa uwezo na nafasi yake ili hospitali ya Wilaya ya Muheza ikamilike mapema.
Mbunge wa Jimbo la Muheza Mhe. Adadi Rajabu alimshukuru Makamu wa Rais kwa kuwezesha kufanikisha kupatikana kwa mchango mkubwa ambao hawakuutegemea na kuahidi ili kuuenzi mchango huu na mapenzi ya  Mheshimiwa Makamu wa Rais kwa wana Muheza basi watahakikisha hospitali hiyo au jengo lolote lile la Hospitali hiyo linapewa jina la Mheshimiwa Makamu wa Rais.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto





Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu