Friday, December 28, 2012

ESSI AONGOZA WALIOZIFUNGIA TIMU ZAO ZA TAIFA MAGOLI MENGI MWAKA 2012... ANAFUATIWA NA ZLATAN IBRAHIMOVICH

ESSI AONGOZA WALIOZIFUNGIA TIMU ZAO ZA TAIFA MAGOLI MENGI MWAKA 2012... ANAFUATIWA NA ZLATAN IBRAHIMOVICH

Lionel Messi

MWAKA 2012, Messi hatimaye amekuwa nyota wa mabao wa Argentina baada ya kushindwa kwa miaka mingi kuhamishia kwenye timu yake ya taifa makali yake ambayo amekuwa akiyaonyesha Barcelona.

Maswali kuhusu tofauti ya kiwango cha Messi awapo Barcelona na anapoichezea timu ya taifa ya Argentina yanaonekana kupata majibu baada ya kuwasili kwa kocha Alejandro Sabella kwenye benchi la ufundi la Argentina.

Messi ndiye aliyeibuka kuwa mfungaji magoli mengi zaidi duniani ndani ya mwaka mmoja 2012 baada ya kufunga mabao 91, huku mabao 12 akiifungia timu ya taifa ya Argentina.

Huku akiwa amempita kwa goli moja Zlatan Ibrahimovic (ambaye ameifungia timu yake ya taifa ya Sweden magoli 11 mwaka 2012), Messi ametangazwa kuwa mchezaji aliyeifungia timu yake ya taifa mabao mengi zaidi katika mwaka 2012, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kabisa kwake kufanya hivyo. Kufikia sasa, takwimu za mabao za nyota huyo wa Barcelona kwenye timu yake ya taifa ya Argentina zimekuwa ni ndogo kulinganisha na zile za klabu.

Mwaka wake bora katika katika ngazi ya taifa ulikuwa 2007, ambapo alifunga magoli sita kwa  Argentina, yakiwamo mawili yake ya kwanza katika mechi moja, ambayo ilikuwa ni ya kirafiki dhidi ya  Algeria.

Magoli 12 ya Messi katika mwaka 2012 yanajumuisha 'hat-trick' zake mbili za kwanza kwa Argentina, alizofunga dhidi ya Brazil na Sweden.

Kama nyongeza, amefunga 'hat-trick' 19 akiwa na Barcelona, maholi manne katika mechi moja na magoli matano katika mechi nyingine moja.

Kutokana na David Villa kuwa mgonjwa baada ya kuumia vibaya Desemba 2011, Pedro ameibuka kuwa kinara wa mabao katika timu ya taifa ya Hispania. Nyota huyo wa Barcelona alikwenda kibahati kwenye fainali za Euro 2012 kutokana na kiwango chake wakati huo kuwa chini, lakini amefunga mabao saba katika mechi nane za timu ya taifa alizocheza mwaka huu.

RADAMEL FALCAO ATWAA TUZO YA MWANASOKA BORA WA MWAKA 2012...NI TUZO INAYOTOLEWA KILA MWAKA NA GLOBE SOCCER... AWAPIKU LIONEL MESSI NA CRISTIANO RONALDO BAADA YA KUWAPIGA CHELSEA HAT-TRICK NA KUIPA ATLETICO MADRID TAJI LA SUPER CUP LA ULAYA... PIA ALIISAIDIA KLABU YAKE ATLETICO MADRID KUTWAA UBINGWA WA LIGI YA EUROPA MWAKA 2012

Radamel Falcao
Natishaaaaaa....! Radamel Falcao akishangilia baada ya kutupia bao.
DUBAI, Falme za Kiarabu
Straika wa klabu ya Atlético de Madrid ya Hispania, Radamel Falcao atakabidhiwa zawadi yake baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka 2012 ya Globe Soccer, ambayo hafla yake inafanyika jijini Dubai leo Desemba 28 na kesho (Desemba 29).

Falcao anayejulikana pia kwa jina la utani la 'The Tiger', alikuwa katika kiwango cha juu mwaka 2012. Alifunga jumla ya magoli 49 na pia kuisaidia Atlético kutwaa mataji mawili. Mcolombia huyu alithibitisha umuhimu wake katika kila michuano baada ya kufunga magoli mawili katika fainali ya Ligi ya Europa na kuipa ubingwa Atletico na pia akapiga 'hat-trick' katika fainali ya kuwania taji la Super Cup la Ulaya dhidi ya Chelsea na kuipa ubingwa klabu yake kutokana na ushindi wa 4-1.

Kwa sababu ya tuzo yake na pia kulazimika kuhudhuria hafla hiyo jijini Dubai, Falcao atachelewa kuanza mazoezi na wenzake klabuni Atlético.

Atlético imepanga kuanza kujifua kesho Jumamosi (Desemba 29) baada ya mapumziko ya Krismasi, lakini Mcolombia huyo anatarajiwa kuungana na kocha wake Simeone na  wachezaji wengine keshokutwa Jumapili (Desemba 30).

Mbali na Falcao, Atlético imeteuliwa pamoja na Chelsea, BATE Borisov na Juventus kuwania Tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka. Miguel Ángel Gil Marín wa Atlético pia yuko jijini Dubai baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Mkurugenzi Bora wa Klabu.

JOSE MOURINHO ATUA DUBAI NA KUSEMA HUU SIYO WAKATI WA KUJADILI HATMA YAKE REAL MADRID... KUKUTANA NA MARADONA, RADAMEL FALCAO, PLATINI

Mourinho (kushoto) akipokewa na wenyeji wake baada ya kutua katika uwanja wa ndege jijini Dubai jana.
DUBAI, Falme za Kiarabu
José Mourinho alitua jijini Dubai jana kushiriki katika mkutano wa saba wa michezo wa kimataifa (Dubai International Sports Conference).

Wakati akiwasili, kocha huyo wa Real Madrid aliulizwa kama ana mpango wa kuendlea kubaki na klabu yake ya sasa. Akajibu: "Sasa si wakati wa kuzungumzia hatma yangu", aliwaambia waandishi wa habari huku akitabasamu.

Mourinho ni miongoni mwa vinara wanaonogesha mkutano huo akiwa pamoja na Diego Armando Maradona, ambaye ndiye mwenyeji, rais wa UEFA, Michel Platini, ambaye ndiye mfunguaji wa mkutano na straika wa klabu ya Atlético de Madrid, Radamel Falcao
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu