2


SI LA KULIKOSA

Wednesday, June 21, 2017

TAIFA STARS WAKIWA KWENYE MAZOEZI JAKAYA KIKWETE

0 comments


MZUKA BLOG

Endelea Kusoma >>

Waziri wa Habari akutana na Wasanii wa Filamu na Waandishi wa Habari wa AFm Dodoma leo

0 comments

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura wakiwa katika picha ya pamoja waandishi wa habari wa A Fm Radio walipomtembelea Bungeni leo Tar 21 Juni 2017.


Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akiwa na waandishi wa habari wa A Fm Radio walipomtembelea Bungeni leo Tar 21 Juni 2017.
Endelea Kusoma >>

SPIKA NDUGAI AFUTURISHA WABUNGE NA WATUMISHI WA BUNGE KATIKA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA.

0 comments
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akizungumza jambo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Joyce Ndalichako (katikati) wakati wa futari aliyoiandaa kwa ajili ya Wabunge na Watumishi wa Bunge iliyofanyika katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, kulia ni Mbunge wa Mbalali Mheshimiwa Haroon Pirmohamed.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akizungumza wakati wa futari aliyoiandaa kwa ajili ya Wabunge na Watumishi wa Bunge iliyofanyika katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, kulia ni Mbunge wa Ilala, Mheshimiwa Mussa Zungu, anaefuata ni Mbunge wa Bariadi Magharibi Mheshimiwa Andrew Chenge na wa pili kushoto ni Mbunge wa Mbalali Mheshimiwa Haroon Pirmohamed.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Mbunge wa Mbalali Mheshimiwa Haroon Pirmohamed (kulia) wakati wa futari aliyoiandaa kwa ajili ya Wabunge na Watumishi wa Bunge iliyofanyika katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa tatu kushoto) akifurahi jambo wakati wa futari aliyoiandaa kwa ajili ya Wabunge na Watumishi wa Bunge iliyofanyika katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, wa pili kushoto ni Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akiagana na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa (kushoto) baada ya kumalizika kwa futari aliyoiandaa jana katika kwa ajili ya Wabunge na Watumishi wa Bunge iliyofanyika katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
Endelea Kusoma >>

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA CHAMA CHA ASKARI WASTAAFU WA VITA KUU YA PILI YA DUNIA LEO OFISINI KWAKE MJINI DODOMA.

0 comments
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akipokea Barua ya kujitambulisha na kuomba msaada wa mchango kwa ajili ya kufanya Mkutano Mkuu wa Chama cha Askari wastaafu kwa Vita kuu ya pili ya dunia waliopigana Mwaka 1939 – 1945 kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama hicho ambae ni Ndg. Bakari Ngonja, katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akutana na kufanya mazungumzo na Chama cha Askari wastaafu wa Vita kuu ya pili ya dunia waliopigana Mwaka 1939 -1945 katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akisisitiza jambo pale alipokutana na kufanya mazungumzo na Chama cha Askari wastaafu wa Vita kuu ya pili ya dunia waliopigana Mwaka 1939 -1945 katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
Endelea Kusoma >>

SPIKA NDUGAI APATA UGENI KUTOKA BUNGE LA MSUMBIJI LEO OFISINI KWAKE MJINI DODOMA.

0 comments

 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akisisitiza jambo mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kutoka Bunge la Msumbiji uliomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, katikati ni Kiongozi wa Msafara na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kutoka Bunge la Msumbiji, Mhe. Lucas Jeremias na kulia ni Mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Beatriz Chagula.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Kiongozi wa Msafara na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kutoka Bunge la Msumbiji, Mhe. Lucas Jeremias (katikati) pale ugeni kutoka kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kutoka Bunge la Msumbiji ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, kulia ni Mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Beatriz Chaguala.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akizungumza  mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kutoka Bunge la Msumbiji ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, wa pili kushoto ni Kiongozi wa Msafara na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kutoka Bunge la Msumbiji, Mhe. Lucas Jeremias
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
Endelea Kusoma >>
0 comments
WAKUU NAOMBA KUWAPA HABARI JUU YA UTALIII WA TANZANIA... ====
Endelea Kusoma >>

Tuesday, June 20, 2017

0 comments
ZIFAHAMU BAADHI YA SEHEMU ZA KITALII JIJINI DAR ES SALAAM z
Na Jumia Travel Tanzania

Umaarufu wa Dar es Salaam kwenye shughuli za kibiashara umelifanya jiji hili kuwa vigumu kwa watu kuvizingatia vivutio vyake vya kitalii. Watu wengi huvifahamu kwa kuviona tu lakini bila ya kujua kihistoria sehemu hizo zina maana sana na wageni huja wakitokea nchi mbalimbali kujifunza.
 
Ukiachana na ufukwe wa Coco Beach unaopatikana pembezeni mwa bahari ya hindi eneo la Oyster Bay, Jumia Travel ingependa kukufahamisha kwamba unaweza kujifunza na kufurahia mambo mengi pindi utakapotembelea maeneo yafuatayo.

Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni. Makumbusho haya awali yalifunguliwa mwaka 1940 kama kumbukumbu ya Mfalme George wa tano ambapo kihistoria huwarudisha watanzania nyuma walipotokea. Makumbusho haya huonyesha mabaki muhimu ya binadamu wa kale yaliyogunduliwa na Dkt. Leakey aliyoyachimbua kwenye bonde la Olduvai. Wageni wanaweza kujifunza urithi wa kitamaduni kutoka kwa makabila mbalimbali Tanzania pamoja na athari za biashara ya utumwa kipindi cha utawala wa kikoloni. Baadhi ya vitu vingine vinavyopatikana katika makumbusho haya yaliyopo mtaa wa Shaaban Roberts ni zana za jadi, desturi, mapambo na vyombo vya muziki.  
 
Kijiji cha Makumbusho. Takribani maili 6 kutokea katikati ya jiji, kuna kiji cha makumbusho ambacho kimehifadhi tamaduni za makabila zaidi ya 120 yanayopatikana Tanzania. Wageni wanaweza kuzunguka kwenye vibanda kadhaa vya nyasi vinavyopatikana pale kwenye ukbwa wa takribani hekari 15 na kujionea ufundi wa kijadi katika kuchora, ufumaji na uchongaji. Kijiji hiki kinachopatikana eneo la Kijitonyama, barabara ya Bagamoyo pia huwa na ngoma na michezo ya jadi pamoja shughuli nyingize za kitamaduni.

Sanamu la Askari. Likiwa limetengenezwa kwa shaba sanamu hili ya Askari huonyesha askari akiwa amevalia vazi rasmi lililotumika kipindi cha vita ya Kwanza ya Dunia huku ncha ya mbele ya bunduki (kama kisu) ikiwa imeelekezwa karibu na bandari iliyopo jirani. Sanamu hili huonyesha kama kumbukumbu ya majeshi ya waafrika walioshiriki kupigana kwenye vita ya Kwanza ya Dunia na linapatikana mtaa wa Azikiwe na Samora.
 
Boma la Kale. Likiwa limejengwa mnamo mwaka 1866 mpaka 1867 na Majid Bin Said, Sultani wa Zanzibar, Boma hili la kale ni jengo lenye umri zaidi ambalo linapatikana kwa sasa jijini Dar es Salaam. Jengo hili lilitumika kuwakarabisha wageni wa Sultani ambaye alikuwa na kasri lake pembeni yake. Vitu vya kuvutia kwenye jengo hili lililopo mtaa wa barabara ya Sokoine ni namna lilivyojengwa kwa ndani vikiwemo mlango wa mbao kutokea Zanzibar na kuta zilizojengwa kutokana na matumbawe.

Kanisa la Mtakatifu Joseph. Jengo hili la Kanisa la Kiroma lilijengwa na wamisionari wa Kijerumani mnamo mwaka 1897 mpaka 1902, kwa kiasi kikubwa ni kivutio kinachoweza kuonekana eneo la karibu na bandarini. Jengo hili kwa ndani limejengwa kwa ufundi na ubunifu wa hali ya juu na kutumia stadi halisi kabiza za kijerumani. Jengo hili ndio Makao Makuu ya kanisa hilo na liinapatikana katika barabara ya Sokoine.   

Kanisa la KKKT Azania Front. Wajerumani walilijenga kanisa la KKKT Azania Front mnamo mwaka 1898. Namna jengo hili lilivyojengwa hususani paa lake kunalifanya kuwa ni nembo ya kivutio jijini Dar es Salaam. Kuna kipindi kanisa hili ndilo lilikuwa kituo kikuu cha shughuli za kimisionari mnamo karne ya 19, kwa sasa ndio makao makuu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania.

Ikulu. Ikiwa imejengwa kwenye miaka ya 1890, jengo la Ikulu ndilo lilikuwa ni makazi ya mwanzo kabisa ya Gavana wa Ujerumani. Mnamo mwaka 1922, Waingereza walifanya maboresho ya jengo hilo maeneo mbalimbali kufuatia kuliharibu katika kipindi cha vita ya Kwanza ya Dunia. Ingawa raia wa kawaida hawawezi kuingia ndani lakini bado linabaki kuwa kivutio kikubwa mtu akipita karibu nalo. Jengo hili linapatikana mtaa wa Luthuli barabara ya kuelekea Kivukoni.   
 
Kisiwa cha Mbudya. Kisiwa hiki kinapatikana umbali wa dakika kumi kwa mwendo wa boti kutokea Kunduchi kikiwa ni hifadhi ya majinii jijini Dar es Salaam. Ukiwa kisiwani hapa utasahau kabisa pilikapilika za katikati mwa jiji hili kwa kufurahia fukwe safi, michezo ya kwenye maji na kuogelea. Kisiwani haoa kuna vibanda vya kukodisha karibu na ufukwe huku vyakula vya baharini pamoja vinywaji vikipatikana pia. Sehemu hii ni maarufu sana kwa watu wanaopenda kutalii kwa siku moja wakitokea katikati ya jiji.

Kisiwa cha Bongoyo. Takribani maili 4 Kaskazini mwa jiji la Dar es Salaam eneo la Msasani kinapatikana kisiwa cha Bongoyo. Kwa wale wanaopenda kusafiri kwa siku moja na kurudi hii sehemu pekee na ya kuvutia ambayo unaweza kufurahia mambo mengi. Kisiwa kina fukwe safi, michezo ya kwenye maji, pamoja na kujionea aina kadhaa za samaki wa baharini. Nyuma ya kisiwa hiki kuna mibuyu mikubwa ambayo huleta hewa safi kwenye fukwe za kisiwa hiko huku vyakula vya baharini na vinywaji hupatikana kwa ajili ya wanaotembelea. Bongoyo kwa sasa inawezekana kuwa ni miongoni mwa visiwa vinne vinavyotembelewa zaidi kwenye hifadhi za maji jijini Dar es Salaam.
 
Dar es Salaam ina mambo mengi ya kujifunza ingawa mengi yamezingwa na shughuli za kibiashara zilizotapakaa kila kona. Jumia Travel inaamini kuwa inawezekana unaishi na vivutio vya kitalii karibu nawe lakini ulikuwa haufahamu. Hivyo basi kabla ya kufikiria kwenda mbali kutalii vivutio vingine anza na vilivyomo jijini hapa kwani vipo karibu nawe na haikugharimu sana kuvitembelea.
Endelea Kusoma >>

WCF YATOA MUONGOZO WA TATHMINI YA UGONJWA NA AJALI KWA MADAKTARI

0 comments
WCF YATOA MUONGOZO WA TATHMINI YA UGONJWA NA AJALI KWA M

Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Emmanuel Humba, akifungua mafunzo ya siku tano kwa madaktari 70 kutoka hospitali 35 za umma na binafsi jijini Dar es Salaam kuhusu namna  ya kufanya tathmini ya ugonjwa na ajali, kabla ya kumlipa fidia mfanyakazi aliyeathirika. Wakwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba na katikati ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulsalaam Omar


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw. Masha Mshomba, (aliyesimama),akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa madaktari kuhusu namna ya kufanya tathmini ya ugonjwa na ajali apatayo Mfanyakazi mahala pa kazi ili taratibu za fidiwa zifanyike. Mafunzo hayo yaliyowaleta madaktari 70 kutoka hospitali 35 za umma na binafsi za jijini Dar es Salaam, yameanza leo Juni 19, 2017. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba, na katikati ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulsalaam Omar


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, umetoa muongozo utakaotumiwa na madaktari na watoa huduma za afya, wakati wa kufanya tathmini ya ugonjwa na ajali kwa mfanyakazi aliyepata madhara mahala pa kazi.
Muongozo huo ni miongoni mwa masuala mbalimbali watakayojifunza madaktari wapatao 70 kutoka hospitali 35 za umma na binafsi za jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo,  Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw  Masha Mshomba, alisema kuwa  madaktari ni wadau muhimu sana  katika kufanikisha shughuli za Mfuko huo.
“Tunataka hawa  madaktari wawe na ujuzi wa kutosha utakaowawezesha kufanikisha azma yetu, na tumeamua kuwa mafunzo ya aina hii yatakuwa endelevu ikiwa ni pamoja na kuwapatia muongozo utakaowasaidia kutekeleza majukumu yao ya kufanya tathmini,” alisema.
Alisema kuwa katika jitihada za kuendeleza mafunzo hayo, Mfuko huo una mpango wa kushirikiana na vyuo vikuu nchini katika kutoa huduma hiyo.
Kuhusu wafanyakazi walioripoti matukio ya ajali kazini  kwenye Mfuko huo hadi hivi sasa, alisema jumla ya kesi 670 za wafanyaakzi walioumia na kuhitaji matibabu zimepokelewa.
Alisema kuwa  wengi wa wafanyakazi waliopatwa na matatizo hayo kazini wanatoka sekta mbali mbali kama migodi, viwanda na usafirishaji. Aliwaomba wafanyakazi walioumia wakiwa kazini kuwasiliana na Mfuko huo ili kuweza kusaidiwa.
Alibainisha kuwa Mfuko umeingia mkataba na watoa huduma za afya kwenye hospitali na  vituo vya  afya  zaidi ya 6,000 nchi nzima ambapo zitahudumia wafanyakazi hao.
Alisema huduma za matibabu zinatolewa kwa mfanyakazi atakayeumia au kuugua kutokana na kazi. Huduma hizo ni ya gari la kubeba wagonjwa, kumuona daktari,upasuaji, uuguzi, dawa, kurudia matibabu itapobidi na kupatiwa viungo bandia.
Alibainisha kuwa wajibu wa mfanyakazi ni pamoja na kuifahamu sheria ya fidia kwa wafanyakazi, (sura 263 marejeo ya mwaka 2015), kutoa taarifa kwa wakati kwa mwajiri au Mkurugenzi Mkuu pindi atakapopatwa na ajali kazini au kubainika kuwa na magonjwa yanayotokana na kazi.
Aliwaomba wafanyakazi hao kutoa ushirikiano pindi wanapotakiwa kufanyiwa uchunguzi wa matibabu, kuzingatia maelekezo yatolewayo na Mamlaka mbali mbali  kuhusu usalama mahali pa kazi, kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbali mbali kuhusu masuala ya fidia kwa wafanyakazi , kutunza kumbukumbu binafsi zinazohusu masuala ya kazi.
Akifungua mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Emmanuel Humba aliwashauri madktari hao kufanya kazi zao kwa weledi zaidi ili kuongeza tija na ufanisi kwa lengo la kuiwezesha sekta hiyo kuongeza wigo wa upana wa  huduma.
Bw. Humba alisema kuwa  azma ya mfuko huo kuwa na mtandao mkubwa wa watoa huduma za afya nchi nzima ambao watasaidia Mfuko kutoa fidia stahiki kwa mfanyakazi aliyepata maradhi au majeraha wakati akitekeleza wajibu wake kazini.
“Nyie ni wadau muhimu sana katika kutuwezesha sisi kufanya kazi zetu vizuri ninawaombeni  mzingatie yote mtakayofundishwa kwenye mafunzo haya  na kuongeza weledi  wenu ,” alisema.
Alisema kuwa watoa huduma hao ndio tegemeo kubwa la kupata taarifa sahihi za mgonjwa pindi anapopata matatizo akiwa kazini, kwani  ndipo utaratibu wa malipo au fidia unapoanzia.
“Lazima mjue kuwa pakitokea tatizo lolote la mfanyakazi kulipwa fidia tutanzia kwenu ili kutupa taarifa sahihi kuhusu wagonjwa wa aina hiyo,” alifafanua.
Aidha Bw Humba aliwataka madaktari hao kusaidia kuwaelimisha wateja wao juu ya huduma mbali mbali zinazotolewa na mfuko huo.
“Mara nyingine unaweza kukutana na mgonjwa akakuuliza kuhusu huduma zinazotolewa na Mfuko huu, ndio maana tumewaita hapa kuwaelezeni  yote, tunaomba mtusaidie kuwaelimisha,” alisisitiza.
Mwenyekiti huyo, aliutaka uongozi wa Mfuko  huo kuangalia namna ya kuyafanya mafunzo hayo kuwa endelevu .
“Ninashauri uongozi wa mfuko kuwa na mafunzo  endelevu ya aina hii, ili kuwakumbushia watoa huduma wetu  waweze kuendena na wakati,” alisema.
Alidokeza kuwa  hadi sasa Mfuko umekwisha endesha mafunzo ya aina hiyo sehemu mbali mbali nchini na kushirikisha madaktari wapatao 359.
“Tulianza  kutoa mafunzo ya aina hii mwaka 2015 ambapo tumewashirikisha madaktari kutoka  Kanda ya Mashariki, Ziwa, Kaskazini na Nyanda za Juu Kusini,”alisema


 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulsalaam Omar, akizungumza kwenye mafunzo hayo
 Sehemu ya madaktari wanaohudhuria semina hiyo
 Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, (kushoto) akiteta jambo na Daktari Bingwa wa upasuaji na majeruhi wa Taasisi ya Mifupa MOI, Dkt. Robert Mhina
 Dkt. Daniel Estomiah Kimaro, kutoka hospitali ya Bochi akizunguzma kwenye mafunzo hayo
 Mtaalamu mbobezi wa masuala ya afya na kazi kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili jijini Dar es Salaam, (MUHAS), Yahya Kishashu, (kushoto), na Daktari bingwa wa upasuaji na majeruhi, kutoka MOI, Dkt.Robert Mhina, wakiwasilisha mada juu ya magonjwa yatokanayo na kazi pamoja na ajali mahala pa kazi.
 Bw. Masha akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo
 Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, (kushoto), Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw.Anselim Peter, Mkuu wa Kitengo mcha Sheria cha Mfuko, Bw. Abraham Siyovelwa, na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Bi. Laura George, wakibadilishana mawazo wakati wa mapumziko ya chai.
 Afisa Uhusiano wa WCF, Bi. Zaria Mmanga, akigawa taarifa mbalimbali zihusuzo mafunzo hayo
 Meneja Madai wa WCF, Bi. Rehema Kabongo, (katikati), akizungumza jambo na Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Bi. Laura George, (kulia) na kushoto ni Afisa Uhusiano wa WCF, Bi. Zaria Mmanga


 Maafisa wa juu wa WCF, bw. Stephen Goyayi, (Kushoto) na Bw. james Tenga, wakiwa kwenye mafunzo hayo

Picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi na uongozi wa WCF

Endelea Kusoma >>
 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu