![]() |
Balozi Dkt. Possi akisalimiana na Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin. |
![]() |
Balozi Dkt. Possi katika picha ya pamoja na Baba Mtakatifu Papa Francis. Wengine ni Afisa wa Ubalozi Bw. Abdul Mhinte, na Mama Balozi, Bi. Sada Mshana. |
![]() |
![]() |
Balozi Dkt. Possi akikabidhi hati za utambulisho kama Balozi wa Tanzania Vatican kwa Baba Mtakatifu Papa Francis.
Balozi
wa Tanzania Dkt. Abdallah Saleh Possi, amewasilisha hati za utambulisho
kwa Baba Mtakatifu Papa Francis, Vatican tarehe 17 Mei 2018. Pamoja na
Ujerumani, Ubalozi wa Tanzania uliopo Berlin pia unahudumia maeneo
mengine tisa ya uwakilishi, ikiwemo Vatican.
Kabla
ya kuwasilisha hati za utambulisho, Balozi Dkt. Possi alipata fursa ya
kukutana na viongozi muhimu wa Vatikani, wakiwemo Askofu mkuu Paul
Richard Gallagher, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje na ushirikiano wa
kimataifa, Askofu Mkuu Angelo Becciu, Katibu Mkuu Msaidizi wa Vatican.
Mabalozi
wengine waliowasilisha hati zao ni pamoja na Balozi Ahmad Naseem
Warraich kutoka Pakistan, Balozi Risto Piipponen kutoka Finland, Balozi
Lundeg Purevsuren kutoka Mongolia, Balozi Retšelisitsoe Calvin
Masenyetse kutoka Lesotho, Balozi Karsten Vagn Nielsen kutoka Denmark,
na Balozi Sulaiman Mohammed kutoka Ethiopia.
Baada
ya uwasilishaji hati, pia Balozi Dkt. Possi alipata fursa ya kukutana
na jumuia ya Watanzania wa Vatican. Dkt. Possi aliwaeleza Watanzania hao
kwamba wana jukumu kubwa la kutumia.nafasi zao kuhakikisha nchi ya
Tanzania inadumu katika misingi ya uadilifu, umoja, na amani ambavyo ni
misingi muhimu ya maendeleo.
0 comments:
Post a Comment