MIKOCHENI CITY YATWAA KOMBE LA DIWANI
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni na Diwani wa Kata ya Mikocheni, Yusuf Mwenda
akikabidhi kombe la Diwani kwa Nahodha wa timu ya Mikocheni City, Abdul
Abdallah baada ya kuibuka mabingwa wa kombe hilo kwa penalti 4-3 katika
mechi ya fainali dhidi ya Mikocheni United iliyofanyika kwenye Uwanja wa
Shule ya Msingi Ushindi, Dar es Salaam.
Mshambuliaji
wa timu ya Mikocheni United Keneth Mutta (kulia) akichuana na Jerry
Santo wa Mikocheni City katika mechi ya fainali ya kombe la Diwani
iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Ushindi, Mikocheni, Dar es
Salaam juzi. City waliibuka mabingwa kwa mikwaju ya penati 4-3.
MAZOEZI YA KUAGA MWAKA 2012 NA KUKARIBISHA 2013
Vijana wa jijini Dar es Salaam kutoka klabu za Jogging mbalimbali wakiwa kwenye mazoezi yaliyoanzia kwenye viwanja vya Tanganyika Pekaz Kawe jana, ambapo mazoezi hayo yaliambatana na bonanza kubwa la kuaga mwaka. Bonanza hilo liliandaliwa na Kawe Jogging.
Mbunge wa
Kinondoni Iddi Azzan akiwapa mazoezi vijana wa vikundi mbalimbali vya
Jogging wakati wa Bonanza la kuaga mwaka lililoandaliwa na Klabu ya
Jogging ya Kawe jijini Dar es salaam
Mbunge wa Kinondoni Idd Azan akishiriki kwenye mazoezi hayo ambayo yalianzia Kawe kuzunguka hadi mbezi kupitia Lugalo na kurejea tena Kawe kwa kupitia Old Bagamoyo road.
RAIS KIKWETE AMJULIA HALI PADRI AMBROS MKENDA ALIYEPIGWA RISASI ZANZIBAR
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Padri Ambros Mkenda wa Kanisa
Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar anayeuguza majeraha katika taasisi ya
mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es salaam
leo Jumamosi Dsemba 29, 2012 kukupigwa risasi sehemu za mdomoni na watu
wasiojulikana mapema wiki hii wakati akisubiri kufunguliwa geti la
nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar akiwa ndani ya gari
aliyokuwa akiendesha akiwa pekee yake. Rais Kikwete amempa Padri Mkenda pole nyingi na kumuombea apate nafuu haraka. PICHA NA IKULU
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Padri Ambros Mkenda wa Kanisa
Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar anayeuguza majeraha katika taasisi ya
mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es salaam
leo Jumamosi Dsemba 29, 2012 kufuatia kupigwa risasi sehemu za mdomoni
na watu wasiojulikana mapema wiki hii wakati akisubiri kufunguliwa geti
la nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar akiwa ndani ya gari
aliyokuwa akiendesha akiwa pekee yake. Rais Kikwete amempa Padri Mkenda pole nyingi na kumuombea apate nafuu haraka.
TBL YAFANIKISHA UPANDAJI MITI 2600 MWANZA
Mgeni rasmi
katika kampeni ya Mradi wa Upandaji Miti jijini Mwanza, Henry Mongi,
akipanda mti wakati wa kampeni hiyo katika moja ya mitaa ya jiji
hilo.Anayeshudia kulia ni Afisa Ubora wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
Caroline Muhonoli na wa pili kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Mkuyuni,
Fasheni Lugo. Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Bia Tanzania. (PICHA NA MDAU BALTAZAR MASHAKA)
Mgeni rasmi
katika kampeni ya Mradi wa Upandaji Miti jijini Mwanza, Henry Mongi,
akipanda mti wakati wa kampeni hiyo katika moja ya mitaa ya jiji
hilo.Anayeshudia kulia ni Afisa Ubora wa TBL, Caroline Muhonoli na wa
pili kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Fasheni Lugo.
Mkurugenzi wa
Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Steven Kilindo,
akifukia udongo kwenye shimo alilopanda mti wakati wa kampeni ya
upandaji miti jijini Mwanza mwishoni mwa wiki..Wanaoshuhudia katikati ni
Meneja Ubora wa kampuni hiyo, Caroline Muhonoli na nyuma ya Kilindo ni
Diwani wa Kata ya Mkuyunim, Lugo Fashen.TBL imetumia zaidi ya milioni 30
kupanda miti 7000 katika mikoa ya Mwanza,Kilimanjaro na Mbeya. Kwa Mkoa
wa Mwanza pekee imetumia sh. mil. 10 kupanda miti 2600.
0 comments:
Post a Comment