Saturday, December 29, 2012

WASIFU WA JOHN MKETO

 kwa niaba ya
Daniel Mshana
Marketing Manager
TANESCO LTD | Umeme Park-Ubungo
P.O.Box 9024 | Dar-Es-Salaam
Landline: +255 222 452 170 | Mobile: +255 784 257 046
website: www.tanesco.co.tz
[cid:image001.png@01CDE426.F45B80A0]


Ndugu habari? Please naomba pokea wasifu wa marehemu, mzee John Keto.

Alizaliwa Tarehe 15 August 1917 huko Muheza, Tanga

Alianza shule ya msingi mwaka 1922 akamaliza masomo ya secondary 1934.

Mwaka wa 1935 akaanza kazi ya ualimu huko St. Andrews Minaki hadi
mwaka 1938 alipo jiunga na chuo cha Makerere huko Uganda hadi mwaka wa
1940.

Baada ya masomo huko Makerere alirudi Minaki, kuendeleya na kazi yake
ya ualimu hadi 1949.

Badaye alienda Edinburgh Univesity kwa shahada ya Uzamili 1950-1954

Alirudi aliajiriwa shule ya secondari minaki 1954- 1958 kama makamu wa
mkuu  wa shule.

Baada ya hapo alichaguliwa kuwa mbunge wa TANU Tanga Province 1958-1960

Baada ya kumaliza nafasi hiyo ali teuliwa na Rais Mw. Nyerere kuwa
mwenyekiti wa Public Service Commission toka 1962 hadi 1964

Baada ya kutumika katika nafasi hiyo aliteuliwa  na \Mwalimu Nyerere
kuwa Post Master General(Director General) wa East African Posts and
Telecomunications makao makuu yakiwa Nairobi, Kenya 1964 hadi 1967.

Ilipoundwa East African Community, makao makuu ya posta yali hamishwa
huko Kampala na akaendeleya na kazi ile hadi 1976 alipo staafu.

Hapo ndiyo aliporudi Muheza kuboresha shule ya secondari Hegongo,
wilaya ya muheza tangu mwaka 1978 hadi 1985 aliporudi Korogwe
kupumzika.





________________________________
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu