![]() |
Wanafunzi wakiwa na mabango leo mjini dodoma. |
hapa wameandamana wakililalamikia Jeshi la Polisi Nchini kwa kushindwa kuthibiti vitendo vya matukio ya ubakajina kulawitiwa yanayofanyika chuoni hapo.
Wanafunzi hao ambao waliandamana umbali wa kilomita tatu leo kutoka chuo
kilipo na kuishia viwanja vya Mwalimu Nyerere walidai wanalenga kufikisha ujumbe kwa jamii kutambua vitendo vya kikatili vinavyofanyika chuoni hapo.
maandamano hayo ambayo yalikuwa yakisindikizwa na
Polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia, yalipita katika mitaa mbalimbali
ya Manispaa ya Dodoma.
Waandamanaji hao ambao mbali na kuimba nyimbo za kulilaumu Jeshi la Polisi kwa
kushindwa kuthibiti vitendo hivyo, pia mabango waliyokuwa wamebeba
yakililaumu jeshi hilo.
Askari jeshi la polisi wakijariobu kuwazuia wanafunzi leo mjini dodoma
0 comments:
Post a Comment