*LULU AKIREJEA RUMANDE BAADA YA MSAJILI WA MAHAKAMA KUTOKUWEPO OFISINI LEO KUKAMILISHA TARATIBU ZA DHAMANA YAKE.
Msanii
wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akitoka katika Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam, leo baada ya Msajili wa Mahakama Kuu kutokuwepo
ofisini na hivyo kurudi rumande hadi kesho tarehe 29/1/2013 atakapoletwa
kwa ajili ya kutimiza masharti ya dhamana ikiwa ni pamoja na
kusalimisha kwa Msajili wa mahakama hiyo hati ya kusafiria, kutotoka
nje ya Dar es Salaam bila ruhusa ya mahakama, kuripoti kwa msajili kila
tarehe 1 ya kila mwezi, kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa
serikali ambao watasaini bondi ya Sh.milioni 20 kila mmoja.
Lulu anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia aliyekuwa msanii
mwenzake marehemu Steven Kanumba.
Gari lililomleta Lulu likiondoka mahakamani hapo.
Lulu akisindikizwa na askari Magereza.
Lulu
akipanda katika gari la Magereza kurudi Rumande, baada ya kukamilisha
taratibu za dhamana hiyo na kukosekana kwa Msajili wa Mahakama Kuu,
mahakamani hapo. Picha na Habari Mseto
0 comments:
Post a Comment