mbunge wa jimbo la morogoro mjini Abdullazizi Abood akitembelea draja |
Miungoni mwa maoneo yaliyolalmikiwa siku za hivi karibuni ni pamoja na maji yanayosambazwa na mamlaka ya maji safi na maji taka yanayotoka katika mabomba kuwa machafu ambapo Mbunge huyo alifanya ziara ya kustukiza katika bwa la mindu na kuagiza uongozi wake kurekebisha hali hiyo kitu ambacho kilifanyika.
Eneo lingine ni pamoja na Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambapo wanachi walilalamikia huduma duni na lugha chafu zinazotolewa na wauguzi kwa wagonjwa na Mbunge huyo kulazimika kufika katika eneo hilo na kushuudia hali hiyo baada ya kuelezwa na wagonjwa walilazwa katika wodi mbalimbali.
Hata hivyo kufuatia hali hiyo ilimlazimu Mbunge huyo kuzungumza na uongozi wa Hospitali hiyo ili waweze kukemea wauguzi wenye tabia hiyo kwani wagonjwa wanahitaji kupewa faraja.
Wakizungumza na Waandishi habari mjini hapa ,wanachi hao wanaoishi maeneo ya kihonda walisema katika kipindi cha takribani mwezi mmoja mamlaka ya majisafi na maji taka Moruwasa bila huruma imekuwa ikiwanywesha maji machafu yenye rangi ya kijani,yanayowasha na yanayotoa povu pindi wanapoyachemsha.
“Nampongeza Abood kwa ziara yake maana zaidi ya mwezi mmoja wananchi tulikuwa tunakunywa maji machafu kupita kiasi hadi kubadilika kuwa na rangi ya kijani na ukiyachemsha yanatoa povu kama maji ya kufulia nguo sasa amejionea uhalali wa malalamiko ya wananchi kuhusu tatizo hili la maji”. alisema Agnes Julius mkazi wa kihonda Magorofani.
Naye Ramadhani Omary mkazi wa Kichangani alisema kuwa utendaji wake umesaidia kutatua kero katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ambako wauguzi wamekuwa wakitoa lugha chafu kwa wagonjwa.
Kwa upande wake Abood alisema kuwa yeye amechaguliwa na wananchi hivyo atahakikisha anatetea na kupigania maslahi ya yao huku akisisitiza kumpa ushirikiano kuweza kufikia malengo hayo.
“ Mimi nimegombea ubunge kwajili ya kutetea maslahi ya wananchi wa Morogoro,hivyo siku zote nitakuwa upande wao “ alisema Abood.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment