WATEJA WA NMB SASA KUWEKA FEDHA KUPITIA M- PESA
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa NMB Mark Wiessing,( kulia) na Ofisa Mkuu wa Biashara-
M-Pesa- Jacques Voogt wakitiliana saini mkataba wa ushirikiano na
makubaliano ya kuwawezesha wateja wa benki ya NMB kufanya muamala wowote
kwenye akaunti zao kwa kutumia huduma ya M-Pesa. Kulia ni Imman Kajula
kutoka Benki ya NMB na (kushoto) ni Kelvin Twisa wa Vodacom, na maofisa
wengine wawili (katikati) pia wakishuhudia.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa NMB Mark Wiessing, (kulia) na Ofisa Mkuu wa Biashara-
M-Pesa- Jacques Voogt wakibadilishana mkataba baada ya kutiliana saini
kama ishara ya ushirikiano na makubaliano ya kuwawezesha wateja wa NMB
kufanya muamala wowote kwenye akaunti zao kwa kutumia huduma ya M-Pesa.
Hafla hiyo ya kutiliana saini kataba huo imefanyika leo jijini Dar es
Salaam.
*************************************************************
BENKI ya NMB
leo imeweka historia kwa kuanzisha huduma mpya itakayowawezesha
wateja wake nchini kote kuweza kuweka amana zao kupitia mawakala zaidi
ya 40,000 wa huduma ya M-Pesa. Pia wateja wa NMB wataweza kutuma fedha
kutoka NMB kwenda MPESA. NMB na Vodacom zimeshirikiana katika huduma
hiyo na kuzindua rasmi huduma hiyo katika hafla fupi iliyofanyika leo
mchana katika Ofisi za Makao Makuu ya Benki hiyo ya NMB, jijini Dar es Salaam.
Baada
ya kuzinduliwa kwa huduma hiyo Sasa mtu yeyote ama wateja wa NMB
hawatahitaji kwenda ndani ya benki ili kuweka fedha kwenye akaunti kwani
sasa wataweza kuweka fedha katika akaunti ya NMB bila kwenda tawini.
Pia sasa wateja zaidi ya 800,000 wa NMB mobile wataweza kutuma fedha
kwenda MPESA.
Akizungumza
wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo, jijini Dar es Salaam, Ofisa
Mtendaji Mkuu wa NMB, Mark Wiessing, “alisema “Ni huduma ya aina yake
ambayo itawezesha mzunguko wa miamala baina ya wateja na benki ya NMB
kufanyika kwa urahisi na haraka, jambo litakalosaidia kwa kiasi kikubwa
kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki sanjari na kuboresha hali
ya maisha na uchumi kwa watanzania wote mijini na vijijini”.
0 comments:
Post a Comment