Thursday, February 28, 2013


*SHEREHE ZA KUMBUKUMBU YA VITA VYA MAJIMAJI 2013 ZAFIKIA KILELE LEO SONGEA


Mheshimiwa  Balozi Hamisi Kagasheki (MB)Waziri wa Maliasili na Utalii akisalimiana na wageni toka Lichinga Msumbiji.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Balozi Hamisi Kagasheki(MB) akisalimiana na Wazee wa Jadi.
Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB) Akivalishwa Vazi la kijadi.
Mhe.Balozi Hamisi Kagasheki (MB)Waziri wa Maliasili na Utalii akiweka Ngao .
 Baadhi ya wazee  wakiwa wameshika Silaha za Jadi walizotumia mababu zetu kupigania dhidi ya kupinga utawala wa Wakoloni wa Kijerumani
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akiweka Sime.
Kamanda wa Jeshi la wananchi akiweka upinde

Mpiganaji wa vita kuu ya pili ya Dunia Mzee Komba akisindikizwa na kamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenda kuweka shahada ya uwa katika mnala wa mashujaa.

 Hii ni kwa nje ndivyo hali ilivyokuwa
 Mhe Balozi Hamisi Kagasheki(MB)Waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na viongozi wengine wakitoa salamu ya heshima kwa mashujaa wa majimaji 
Hapo wanajeshi wakiendelea kutoasalamuza maombelezi kwa njia ya kijeshi
   Kuinamisha kichwa chini ni dalili ya kumwomba mwenyezi Mungu awaweke Mahali pema Mashujaa  walioo tangulia Mbele zahaki
Katika kuwakumbuka Mashujaa waliotangulia mbele za Haki Jeshi la Wananchi limeweka Utaratibu Maalumu ikiwa ni pamoja na kulipua mizinga na Fataki katika kuwakenzi Mashujaa.
Jeshi la Wananchi wa Tanzania likitoka nje ya Uwanja wa Mashujaa baada ya kumaliza taratibu zote za Maombolezo.  
 Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mzuri  na wakuelimisha juu ya vita vya majimaji.

 Moja ya wageni waliohudhuria toka mikoa mbalimbali pamoja na nchi jilani ya Mozambiq

 Chief Emanuel Zulu akiweka shada katika kaburi la pamoja la mashujaa wa vita vya majimaji.
Hili ndilo Kaburi la halaiki walipozikwa mashujaa wa vita vya Maji Maji , watu waliozikwa hapa ni 66
Eneo hili walilozikwa mashujaa hawa limekuwa eneo muhimu.
Mhe.Balozi Hamisi Kagasheki akipewa maelezo juu ya Kaburi la Songea Mbano ambaye alizikwa peke yake na jina la Mji wa Songea limetokana na jina lake

Balthazar Nyamusya Mhifadhi Kiongozi wa Makumbusho Ya Taifa Maji Maji Sonhgea akitoa maelezo kwa 
Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB) alipokuwa akizuru ukumbi wa historia ya vita vya maji maji.Miongoni mwa vionyeshwa katika ukumbi wa historia ni zawadi iliyokabidhiwa na MeyaAugusto Assique wa Jimbo la Lichinga kwa kutambua mashirikiano ya kihistia na kitamaduni. Picha zote na Hamza Mashole

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu