Friday, March 29, 2013

KUAGA MWILI WA ALIEKUWA MBUNGE WA CHAMBANI SALIM HEMED KHAMIS LEO

.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri Mstaafu, Edward Lowasa, na viongozi wengine wakishiriki shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia CUF, aliyefariki jana mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zimefanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Machi 29, 2013. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya ndugu wa marehemu wakati viongozi wakiondoka kwenye ukumbi wa Karimjee baada ya kushiriki katika shughuli za kuaga mwili wa marehemu, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba, Salim Hemed Khamis (CUF), aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) William Lukuvi, na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Adam Malima, wakizungumza nje ya ukumbi wa Karimjee, baada ya kushiriki shughuli ya kuaga mwili wa marehemu,Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia Chama cha CUF, aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu,Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia Chama cha CUF, aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakiingiza kwenye gari tayari kuelekea uwanja wa ndege kwa safari ya kuelekea Pemba kwa maziko, yatakayofanyika leo. 

*BREAKING NEEEWZ!!! JENGO LA GHOROFA 14 LAPOROMOKA DAR LAFUKIA WATU KADHAA

 Jengo la Ghorofa 14 lililokuwa likiendelea kujengwa pembeni kabisa mwa Msikiti wa SHIA Mtaa wa INDRA GHAND na Zanaki, limeporomoka na kusambaratika na kusababisha vifo vya watu kadhaa ambao hadi sasa idadi haijaweza kupatikana kutokana na waokoaji kukosa vifaa vya kutosha katika zoezi hilo la uokoaji. Imeelezwa kuwa ghorofa hilo limeporomoka leo asubuhi majira ya saa moja na nusu ambapo ulianza kusikika mlio kama 'Tetemeko la ardhi'. 
Aidha imeelezwa kuwa katika Jengo hilo walikuwepo mafundi ambao walikuwa wakiendelea na ujenzi na chini alikuwepo Mama Lishe, aliyekuwa akiuza chai na eneo hilo pia walikuwapo watoto wadogo ambao haikuweza kufahamika idadi yao waliokuwa wakicheza eneo hilo, ambao wote inasemekana wamefukiwa na kifusi cha ghorofa hilo, huku waokoaji wakifanikiwa kumpata mtoto mmoja tu ambaye hata hivyo imeelezwa hali yake ilikuwa ni mbaya na kuwahishwa hospitali.
 Ni moja ya Kifaa pekee kilichokuwepo eneo hilo Trekta, likifukua kifusi ili kuokoa watu wanaodaiwa kufukiwa na kifusi hicho.
 Baadhi ya watu waliwahi kufika kujaribu kutoa msaada bila mafanikio hapa wakiwa wamekwama baada ya kukosa vifaa vya kutosha.
 Wahindi nao walikuwapo kutoa msaada hapa wakilielekeza Trekta kusogea mahala walipo wao wakihisi kuwa kuna mtu mahala hapo.
 Waokoaji wakijitahidi kutumia mikono kuondoa kifusi hicho ili kuweza kuwaokoa watu waliofukiwa.
 Trekta likiendelea kuondoa kifusi hicho.
 Waokoaji wakiwa hoi......
 Juhudi zinaelekea kulala.........
 Moja kati ya magari yaliyokuwa eneo hilo likiwa limeangukiwa na mabaki ya jengo hilo.
 Trekta likiendelea kuondosha kifusi......../
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik, akihojiwa na wanahabari kuhusu tukio hilo.
 Moja ya ghorofa lililo karibu kabisa na jengo hilo lililoanguka nalo likiendelea kujenga nalo pia likiwa na ghorofa 14.....
 Sehemu ya wananchi wakishuhudia tukio hilo.
Vijana wakishusha mitungi ya gesi ili kuwasaidia kukata nondo.... baada ya kuona vimekosekana vifaa vya haraka.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu