Friday, March 29, 2013

MAITI ZAIDI YA 10 NA MAJERUHI 30 TU WACHOMOLEWA HADI SASA KATIKA MABAKI YA JENGO LA GHOROFA 16 LILILOPOROMOKA JIJINI DAR ES SALAAM LEO ASUBUHI HII NA KUWAFUNIKA WATU KIBAO WAKIWAMO MAFUNDI WALIOKUWA WAKIENDELEA KULIJENGA... NI JIRANI NA MSIKITI WA SHIA MAKUTANO YA MOROGORO ROAD NA INDIRA GANDHI... HARAKATI ZA KUCHOMOA MAJERUHI NA MAITI ZAIDI ZINAENDELEA ZIKIONGOZWA NA VIONGOZI KADHAA WA SERIKALI AKIWAMO RC DAR, SAID MECK SADICK

Mashuhuda wakiangalia jengo lililoporomoka asubuhi hii katika makutano ya Morogoro Road na Indira Gandhi jijini Dar es Salaam leo asubuhi Machi 29, 2013.
Maafa makubwa yametokea jijini Dar es Salaam leo baada ya jengo la ghorofa 16 lililokuwa likiendelea kujengwa kuporomoka na kuwafunika watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 6o

Tukio hilo limetokea mishale ya asubuhi katika mitaa ya Posta, jirani na msikiti wa Shia katika eneo la makutano ya Morogoro Road na Indira Gandhi na hadi sasa, miili ya maiti 12 na pia majeruhi 30 wameshachomolewa.

Aidha, harakati zaidi za uokoaji zingali zikiendelea kufanywa na vikosi vya uokoaji. Katika eneo la tukio hilo, tayari viongozi kadhaa wa serikali na makamanda wa Polisi katika kanda maalum ya Dar es Salaam wamefika kusaidia shughuli za uokoaji, miongoni mwao akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick.

Baadhi ya mashuhuda wamedai kuwa mabaki ya jengo hilo yanaonyesha kuwa mchanga ulikuwa mwingi mno kulinganisha na saruji, hali inayodhaniwa kuwa ni miongoni mwa sababu za kuporomoka kwa mjengo huo uliogharimu mamilioni ya pesa.

Hadi kufikia sasa, hakuna taarifa rasmi za serikali zilizotolewa kuelezea msiba huo
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu