MHASHAMU Askofu wa kanisa Katoriki jimbo la Morogoro Telesphori Mkude,akihutubia mamia ya waumini wa kanisa hilo katika ibada pasaka ya kuzaliwa kwa Yesu kristo iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Patriki Mjini Morogoro,
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Sewa haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Machi 31, 2013 wakimjulia hali na kumpa pole Bw. Selemani Saidi, mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 28 Kushoto mwenye suti nyeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Raymond Mushi Kulia ni Daktari C.N. Mcharo wa taasisi ya Mifupa ya Moi.
Baadhi ya watu mbalimbali waliofika katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa aajili ya kutambua ndugu zao waliokufa kwa ajali ya kuangukiwa na ghorofa
Baadhi ya waumini wa kanisa la St Joseph jijini Dar es salaam wakitoka katika ibada ya Pasaka leo
Muuguzi mkunga Fatuma Uwesu wa Hospitali ya Mwananyamalakulia akimpa chanjo mtoto ambaye aliezaliwa katika mkesha wa pasaka kushoto ni mama wa mtoto huyo Maria Weus leo
Masita wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dodoma wakisikiliza mahubiri ya Askofu Gervas Nyaisonga jana katika kanisa la Mt Paulo wa Msalaba Dodoma mjini
Askofu mkuu wa kanisa la Injili la KKKT Dr Alex Malasusa akimbariki mtoto wakati wa ibada ya Pasaka leo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwasili katika wodi ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kuwajulia hali vijana Mohamed Ally Dhamji (kushoto), Baqir Virani, ambaio ni kati ya majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 28 mpa leo
Baadhi ya waumini wa kikristo wa kanisa la kkkt la Azania wakielekea katika kutoa sadaka wakati wa ibada ya Pasaka leo
0 comments:
Post a Comment