Thursday, April 25, 2013

REAL MADRID KAMA BACELONA YACHEZEA KICHAPO 4-1 NA DORTMUND, MOURINHO HOI

 MABAO manne ya Robert Lewandowski usiku huu yameipa Borussia Dortmund ushindi wa 4-1 dhidi ya Real Madrid katika Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya nchini Ujerumani.

Mabao hayo ya mshambuliaji huyo wa Poland yanawafanya Dortmund watengeneze mazingira ya fainali ya klabu za Ujerumani tupu itakayopigwa Uwanja wa Wembley mwezi ujao, kufuatia jana Bayern Munich kuichapa 4-0 Barcelona nchini Ujerumani pia.
Lewandowski alifunga bao la kwanza dakika ya nane, kabla ya Cristiano Ronaldo kuisawazishia Real dakika ya 43.
Lakini mshambuliaji huyo akarudi na makali zaidi kipindi cha pili na kufunga mabao matatu zaidi dakika za 50, 55 na 67 kwa penalti.
Kocha wa Real, Mreno Jose Mourinho aliyekuwa 'hoi' uwanjani baada ya kipigo leo, sasa anatakiwa kutengeneza mipango ya kushinda 3-0 katika mchezo wa marudiano wiki ijayo, ili kuwapiku Dortmund.
Kikosi cha Borussia Dortmund kilikuwa: Weidenfeller, Piszczek/Grosskreutz dk83, Subotic, Hummels, Schmelzer, Bender, Gundogan/Schieber dk90, Blaszczykowski/Kehl dk82, Gotze, Reus na Lewandowski.
Real Madrid: Diego Lopez, Sergio Ramos, Varane, Pepe, Fabio Coentrao, Khedira, Alonso/Kaka dk80, Ozil, Modric/Di Maria dk68, Ronaldo na Higuain/Benzema dk68.
On fire: Robert Lewandowski scored all four goals as Dortmund crushed Real Madrid in their semi-final first leg
Moto: Robert Lewandowski amefunga mabao yote manne ya Dortmund dhidi ya Real Madrid leo
Perfect start: Lewandowski put Dortmund ahead as early as the eighth minute
La kwanza: Lewandowski akiifungia Dortmund bao la kwanza
Lead: Lewandowski peeled away at the far post to guide Mario Gotze's cross into the far corner
Lewandowski Robert Lewandowski AKISHANGILIA BAO
Level: Cristiano Ronaldo equalised for Real Madrid just before half-time
La kusawazisha: Cristiano Ronaldo aliisawazishia Real Madrid na kipindi cha kwanza kiliisha 1-1
Level: Cristiano Ronaldo equalised for Real Madrid just before half-time
Ahead again: Lewandowski held off Raphael Varane's challenge to give the Germans a 2-1 lead
La pili: Lewandowski akifunga la pili
Lewandowski
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu