Sunday, April 28, 2013



THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Kenya, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta kuomboleza kifo cha Mjumbe wa Baraza la Seneti na Waziri muhimu wa zamani wa nchi hiyo, Mheshimiwa Mutula Kilonzo, aliyefariki dunia juzi, Ijumaa, mjini Nairobi.
Katika salamu zake za rambirambi, Rais Kikwete amemwambia Rais Kenyatta kuwa amepokea habari za kifo cha ghafla cha mwanasiasa huyo kwa mshtuko na huzuni na kuwa kifo chake kimeipokonya nchi hiyo mmoja wa viongozi waliokuwa wanajali na kutanguliza maslahi ya Kenya na wananchi wake.
“Kwa hakika, kifo cha Mheshimiwa Mutula Kilonzo kimeipokonya Kenya kiongozi muhimu. Mchango mkubwa aliuotoa katika kipindi cha kuivusha Kenya kutoka kwenye changamoto za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007 hadi sasa ambako nchi imetulia na inasonga mbele, kamwe hautasahaulika,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Katika nafasi zote za Uwaziri alizozishikilia katika kipindi hicho, kwanza kama Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba na baadaye kama Waziri wa Elimu, alijithibitisha na kujipambanua kama Mzalendo wa kweli kweli wa Kenya na mpenzi halisi wa nchi yake.”
Ameongeza Rais: “Nakutumia Mheshimiwa Rais salamu zangu za rambirambi na zile za Serikali yangu kufuatia msiba huu. Aidha, kupitia kwako naomba unifikishie salamu zangu kwa familia ya Mheshimiwa Kilonzo. Nataka wajue kuwa niko nao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na naungana nao kuomboleza na kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Mutula Kilonzo.Amin.”

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU,
DAR ES SALAAM
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu