Wednesday, May 29, 2013

Nyota wa Bongo Fleva, Albert Mangwea maarufu kama Ngwair, afariki dunia





Na Mwandishi Wetu, IMEWEKWA MEI 29, 2013 SAA 1:30 MCHANA  BLOG YA BIN ZUBBERY
.
Nyota wa Bongo Fleva, Albert Mangwea maarufu kama Ngwair, alifariki dunia jana jioni akiwa nchini Afrika Kusini kutokana na kuzidiwa na matumizi ya dawa za kulevya. Wakati mwili wake unakimbizwa hospitali ya St Hellen Joseph, rafiki yake naye, msanii pia M To Te P alikuwa katika hali mbaya, pia kwa utumiaji wa dawa za kulevya ambako hadi sasa amelazwa kwa matibabu na taarifa zinasema anaendelea vizuri.
Kaka wa marehemu Ngwair, Kenneth Mangwea amesema msiba upo Mbezi Beach, Goigi mjini Dar es Salaam na taratibu za kuirejesha miili ya marehemu nyumbani zimeanza.
Kimuziki, Ngwair aliibukia mkoani Dodoma ambako alikuwa katika kundi moja na Dark Master, Noorah na Mez B na amekuwa akishirikiana na M To The P tangu akiwa msanii anayechipukia baada ya kuhamia Dar es Salaam.
Baada ya kuja Dar es Salaam, Ngwair akapata dili Bongo Records chini ya mmiliki wa studio hizo, Petter Matthysse ‘P Funk’ aliyemuinua zaidi kimuziki na kumfanya awe miongoni mwa wanamuziki nyota nchini.
Wimbo wake wa kwanza kutamba ni Gheto Langu mwaka 2003 ambao ulimpatia umaarufu kabla ya kutoa albamu yake ya kwanza a.k.a Mimi mwaka 2003 ambayo ilimpatia mafanikio makubwa na kubadili maisha yake.
Hata hivyo, mafanikio hayo yalimlevya na kujitumbukiza kwenye utumiaji wa dawa za kulevya, hivyo kujikuta akishindwa kufanya kazi ya muziki kwa usanifu na kuanza taratibu kufilisika hadi kuuza mali zake zote, ikiwemo gari aina ya Jeep.
Ngwair kutoka kwenye kupanga nyumba nzima maeneo ya Sinza, Dar es Salaam akajikuta anarejea kuishi katika ‘magheto’ ya washkaji zake sehemu mbalimbali Dar es Salaam.
Mwaka 2010, Athumani Tippo, mmiliki wa maduka ya Zizzou Fashions alijaribu kumuinua tena msanii huyo baada ya kumchukua kwenye lebo yake na kumuwezesha kutoa albamu ya pili, Nge.
Hata hivyo, Nge haikufanya vizuri sana na kuzidi kumchanganya msanii huyo hivyo kutopea kwenye dimbwi la utumiaji wa dawa za kulevya na ‘kuharibika zaidi’.  
Mafanikio yake zaidi ni kushinda tuzo ya Kilimanjaro Music Awards kama mwana Hip Hop Bora wa mwaka 2005. 
Mwaka 2003, msanii Wayne Wonder aliyekuja kutumbuiza kwenye Fiesta aliondoka na CD ya wimbo Mikasi ya Ngwair baada ya kuvutiwa na kibao hicho alichowashirikisha Mchizi Mox na Ferooz. 
Ngwair alijaribu sana kumuinua kimuziki M, lakini pamoja na ukweli kwamba alikuwa ana kipaji, lakini hakufanikiwa, ingawa aliwahi kutoa albamu Blog ya Bin Zubbery

KUTOKA KWA MWENYEJI WA MAREHEMU NGWEA UKO SOUTH AFRICA SIKILIZA SABABU ZILIZOPELEKEA KIFO CHAKE

Kuna taarifa kuwa chanzo cha kifo cha ghafla cha rapper Mangweir ni kuzidisha madawa ya kulevya aliyotumia usiku wa kuamkia jana.
Hussein Original ambaye yupo Pretoria amesema Ngwear na M to the P ambaye walikuwa room moja wamekutwa wamezima baada ya kuzidhisha madawa ya kulevya...
Hata hivyo mwenyeji wa rapper Albert Mangwea aliyefariki leo jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini, amesema hit maker huyo wa Mikasi amefariki akiwa usingizini.

Akiongea na mwandishi wetu muda mfupi uliopita, mwenyeji huyo aitwaye Jonathan amesema usiku wa kuamkia leo Mangwair alirudi nyumbani alikofikia akiwa mzima wa afya lakini mpaka kunakucha hakuonesha dalili za kuamka.

Ameongeza kuwa asubuhi kulipokucha aliondoka na kuendela na mishemishe yake na alipokuwa huko wenzake walimpigia simu kumtaarifu kuwa wamempeleka hospitali ya St. Helen ya jijini humo kwakuwa alikuwa bado hajaamka na ndipo walipogundua kuwa ameshafariki.
Jonathan amesema hakuweza kujua sababu za kifo cha Ngwair kwakuwa maelezo ya daktari yalikuwa kitaalam kiasi cha kushindwa kuelewa. Ngwair alikuwa amepanga kurudi leo nchini.

 
HISTORIA YAKE


JINA LAKE HALISI NI ALBERT KENETH MANGWAIR,NI MTU WA RUVUMA MNGONI...,,,,MNGONI,LAKINI ALIZALIWA MBEYA TARE
HE 16 NOVEMBER,MWAKA 1982.

YEYE NI MTOTO WA MWISHO KWAO,KWA BABA AKIWA MTOTO WA 10,KWA MAMA AKIWA MTOTO WA 6.

NGWAIR ASILI YAKE NI RUVUMA,YAANI MNGONI, ALIZALIWA MBEYA,A KIWA MIAKA 5 WALIHAMIA MOROGORO AKASOMA SHULE YA MSINGI BUNGO HADI DARASA LA 5,BABA YAKE AKAPATA UHAMISHO AKAHAMIA DODOMA,SO AKAHAMA NA BABA YAKE AKAENDA AKAMALIZA SHULE YA MSINGI MLIMWA DODOMA.BAAADAE MAZENGO SEC,THEN CHUO CHA UFUNDI MAZENGO
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu