Wednesday, July 17, 2013

KAPOMBE ANAONDOKA KESHO MWANZA KWA SAFARI YA UHOLANZI, STARS YAENDELEA KUJIFUA KIRUMBA

Na Prince Akbar, IMEWEKWA JULAI 17, 2013 SAA 2:30 USIKU
KIUNGO wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Shomary Kapombe anaondoka Mwanza kesho asubuhi kuja Dar es Salaam tayari kwa safari ya Uholanzi kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa huko.
Kapombe amelazimika kuiacha kambi ya Stars mjini Mwanza inayojiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda wikiendi ijayo mjini Kampala, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za CHAN mwakani kwa ajili ya safari hiyo.
Kiungo wa Taifa Stars, Frank Domayo akimtoka Shomary Kapombe kwenye mazoezi ya Stars jioni leo Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. 


Domayo anapasua...

Chuji hajang'atuka; Kiungo Athumani Iddi 'Chuji' (wa tatu kushoto) aliyeripotiwa na gazeti moja kwamba ameng'atuka Stars akiwa mazoezini na wenzake leo

Kapombe, anayechezea klabu ya Simba ya Dar es Salaam ataondoka nchini Ijumaa kwenda Uholanzi kujaribu bahati yake, ambako amealikwa na mtu aliyejitolea kumtafutia timu ya kuchezea huko.
Stars inaendelea na mazoezi mjini Mwanza na kocha Kim Poulsen pamoja na kutoa ruhusa Kapombe aende Uholanzi, lakini hajaita mtu wa kuziba pengo lake. 
Tayari kiungo wa Simba SC, Mwinyi Kazimoto ametoroka kwenye kambi hiyo na inadaiwa amekwenda Qatar kutafuta timu, lakini huyo pengo lake limezibwa na Mudathir Yahya wa Azam FC
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu