Saturday, August 31, 2013

MTWARA WAIPOKEA KWA SHANGWE SEMINA YA FURSA KWA VIJANA


Meneja Kiongozi,Uhusiano NSSF Makao makuu jijini Dar, Eunice Chiume  akizungumza mapema leo kwenye semin ya FURSA iliyofanyika kwenye ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana Mtwara,kulia ni Meneja wa NSSF mkoani Mtwara Bwa.Stanley Mullanzi na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iramba (ambaye pia ni mzaliwa wa Newala mkaoni Mtwara),Mh.Yahya Nawanda wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini humo.Semina hiyo inaratibiwa na Clouds Media Group na kufadhiriwa na NSSF,Lake Oil,Zantel,MaxMalipo na wengineo imewashirikisha wadau mbalimbali wa Mtwara na vitongoji vyake wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya.
  Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Mtwara na vitongoji vyake wakifuatilia kwa makini  yaliyokuwa yakijiri kwenye semina ya Fursa kwa Vijana iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa  Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana mkoani Mtwara.
 Mkuu wa Wilaya ya Iramba (ambaye pia ni mzaliwa wa Newala mkaoni Mtwara),Mh.Yahya Nawanda akizungumza na wakazi wa mji wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kwenye semina ya Fursa kwa Vijana mapema leo,Mh.Yahya alizunguma mengi zikiwemo fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya mkoa wa Mtwara na Singida namna ya kuzifanyia kazi katika suala zima la kujikwamua na maisha. 
Mkurugenzi wa Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba  akihitimisha semina ya Fursa kwa Vijana mapema leo mchana,ndani ya ukumbi wa ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana Mtwara,kulia kwake ni Meneja Kiongozi,Uhusiano NSSF Makao makuu jijini Dar,Eunice Chiume pamoja na Meneja wa NSSF mkoani Mtwara Bwa.Stanley Mullanzi.Semina ya Fursa kwa vijana tayari imekwishafanyika mikoa ya Tabora,Kigoma,Singida na sasa Mtwara.
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPO.COM

WAJUMBE WA BARA WAENDA ZANZIBAR KWENYE BARAZA KUU LA UMOJA WA VIJANA WA CCM, TAIFA

 Baadhi ya wajumbe wakiwa Makao Makuu ya UVCCM, jijini Dar es Salaam, tayari kwa safari ya kwenda Zanzibar kwenye kikao cha Baraza Kuu ya Jumuia hiyo, kitakachofanyika kesho.
 Wajumbe wakiwa nje za jengo la Umoja wa Vijana wa CCM, mjini Dar es Salaam, kabla ya kuanza safari yao kwenda Zanzibar
 Baadhi ya wajumbe wakiwa Ofisi za UVCCM mjiniu Dar es Salaam, kabla ya kuondoka kwenda Zanzibar kwenye kikao hicho.
 Wajumbe wakiwa kwenye ofisi ya UVCCM makao makuu
Baadhi ya wajumbe wakipanda mabasi kutoka makao makuu ya UVCCM kwenda Bandarini kubanda boti kwenda Zanzibar kwenye kikao hicho cha Baraza Kuu la UVCCM leo
Baadhi ya wajumbe wakiwa bandari ya Dar es Salaam, kupanda boti
Wajumbe wakiwa kwenye boti mjini Dar es Salaam, tayari kwa safari ya Zanzibar
Wajumbe wakiwa kwenye boti yatari kwa safari ya Zanzibar. Imetayarishwa na theNkoromo Blog
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu