Sunday, September 22, 2013

Paulinho alibeba Spurs ugenini, Man Utd ikilala 4-1

Sergio Aguero of Manchester City (16) celebrates as he scores their first goal during the Barclays Premier League match between Manchester City and Manchester United (Getty Images)
Kun Aguero akishangilia moja ya mabao yake ya leo yaliyoizamisha Manchester United
Wayne Rooney akiwa hoi

Paulinho
BAO la dakika za lala salama lililofungewa na Paulinho liliisaidia Tottenham Hotspur kupata ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Cardiff City, huku Manchester United chini ya kocha wake David Moyes ikilala kwa mahasimu wao Manchester City kwa mabao 4-1.
Paulinho alifunga bao la Spur dakika ya tatu za nyongeza kabla ya mchezo huo kumalizika na kuipa timu yake pointi tatu muhimu zilizoifanya waende sambamba kileleni mwa msimamo na Arsenal iliyoshinda mapema mabao 3-1 dhidi ya Stoke City, japo inazidiwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa licha ya zote kufikisha jumla ya pointi 12.
Mabingwa watetezi Manchester United walijikuta wakipata kipigo cha aibu ikiwa na kocha wake David Moyes baada ya kunyukwa mabao 4-1 na Manchester City.
Mabao mawili ya Sergio 'Kun' Aguero, Yaya Toure na samir Nasir yalitosha kuipandisha City hadi nafasi ya tatu ikifikisha pointi 10 sawa na za Chelsea lakini ikiwa na uwianoi mzuri wa mabao ya kufunga na kufunga ikizipumulia Tottenham na Arsenal zilizopo kileleni.
Bao pekee la kufutia machozi ya Manchester United lilifungwa na nyota wake aliye katika kiwango cha juu kwa sasa Wayne Rooney

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu