Friday, November 29, 2013

Rais Dkt. Jakaya Kikwete apewa Uchifu wa Bariadi

D92A6333Mmoja wa machifu wa Kisukuma eneo la Bariadi ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Mashariki Andrew Chenge akimvika vazi la kijadi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya kumpa uchifu Rais Kikwete iliyofanyika mjini Bariadi,Mkoa mpya wa Simiyu leo.Rais Kikwete alipewa jina la kisukuma la Chifu Ng’humbu Banhu lenye maana ya Anayekumbuka na kuthamini Watu. D92A6385Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amekalia kigoda cha Uchifu wa Bariadi baada ya kuwa Chifu Ng’humbu Banhu mjini Bariadi Mkoa mpya wa Simiyu leo.Rais Kikwete yupo katika Ziara ya Kikazi Mkoa mpya wa Simiyu(picha na Freddy Maro)
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu