WAREMBO WAANZA KUJINOA TAYARI KWA SHINDANO LA MISS TANZANIA USA PAGEANT JUMAMOSI NOV 30
Lady
Kate mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Africa USA Pageant akiwaasa
Mamiss Tanzania USA Pageant leo Jumamtano Novemba kwenye hotel ya
Marriott
Pamela Egbe Messy mratibu wa Miss Africa USA Pageant akiwaelimisha walimbwende
MaWinny
Casey Mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Tanzania USA Pageant katika
picha ya pamoja na mratibu wa Miss Tanzania USA Pageant, Asha Nyang'anyi
(kulia)
Mamiss
Tanzania USA Pageant wakimsikiliza Lady Kate mkurugenzi na mwanzilishi
wa Miss Africa USA Pageant alipokuwa. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
*MTANZANIA CLARA NOOR AANZA KUNG'ARA MASHINDANO YA MISS EARTH UFILIPINO
Mwandishi Wetu
Nyota
wa mrembo wa Tanzania anayewania taji la Miss Earth, Clara Noor imeanza
kung’ara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika taji la fukwe ya
Pagudpud iliyopo nchini Phillipines.
Mbali
ya kutwaa taji hilo, Clara pia ameibuka mshindi wa tatu katika taji la
vazi la Taifa na kuzipiku nchi nyingine nyingi na kuzawadiwa medali ya
shaba.
Katika
mashindano ya tuzo maalum, jumla ya tuzo 11 zilikuwa zinagombaniwa na
warembo 88 walikuwa wanawania mataji hayo ambayo zawadi zake zilitolewa
na wadhamini hao.
Clara
alionyesha uwezo mkubwa katika taji hilo na kuwa mwafrika wa kwanza
kushinda katika historia. Katika vazi la Taifa, Clara aliwavutia wengi
na kupata ushindani mkubwa kutoka kwa mrembo wa warembo kutoka Afrika
Kusini, Ashanti Mbanga na kutoka Nigeria, Marie Miller ambao walishika
nafasi ya kwanza nay a pili.
Muandaaji
wa Miss Earth Tanzania, Maria sarungi Tsehai alisema kuwa ni faraja
kubwa kwa Clara kuitangaza Tanzania kwa kupitia mataji hayo mawili kwani
mbali ya jina lake, kinachotangazwa pia ni nchi.
“Amefanya
vyema mpaka sasa, tunatarajia kuona anaendelea kufanya vizuri na
kutuletea sifa, mpaka sasa anastahili pongezi,” alisema Maria ambaye ni
Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications.
Alisema
kuwa fainali ya mashindano hayo yatafanyika Desemba 7 kwenye ukumbi wa
Versailles Palace, Alabang, Muntinlupa City na kurushwa live na vituo
vya televisheni vya STAR World, ABS-CBN, Velvet, The Filipino Channel,
Ustream na VenevisiĆ³n.
*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA SHEREHE ZA MAADHIMISHO MIAKA 10 YA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA), DAR ES SALAAM.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi msaidizi Chumba cha Mtambo wa
Kufuatilia Mawasiliano ya Simu (Telecommunicatins Traffic Monitoring
System) Sunday Richard, wakati alipotembelea chumba hicho baada ya
kufungua rasmi Sherehe za uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo katika ukumbi wa Mliman City jijini
Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
Prof.Makame Mbarawa (wa pili kulia) ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Mawasiliano (TCRA), Prof. John Nkoma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisoma hituba yake ya uzinduzi rasmi wa sherehe za maadhimisho ya
miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Miaka 10 ya
Mapinduzi katika Sekta ya Mawasiliano Tanzania, yaliyozinduliwa rasmi
leo katika Ukumbi wa Mliman City,jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka ya Mawasiliano TCRA,akizungumza......
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof.Makame Mbarawa,akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais.
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria ufunguzi huo....
Baadhi ya wageni waalikwa na wadau wa mawasiliano wakiwa ukumbini humo....
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijili meza kuu.
Wadau.....
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano
(TCRA), Prof. John Nkoma, wakati alipotembelea katika chumba cha Mtambo
wa Kufuatilia Mawasiliano ya Simu (Telecommunicatins Traffic Monitoring
System) baada ya kufungua rasmi Sherehe za uzinduzi wa Maadhimisho ya
Miaka 10 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo katika ukumbi wa
Mliman City jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia, Prof.Makame Mbarawa.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi msaidizi Chumba cha Mtambo wa
Kufuatilia Mawasiliano ya Simu (Telecommunicatins Traffic Monitoring
System) Sunday Richard, wakati alipotembelea chumba hicho baada ya
kufungua rasmi Sherehe za uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo katika ukumbi wa Mliman City jijini
Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
Prof.Makame Mbarawa (wa pili kulia) ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Mawasiliano (TCRA), Prof. John Nkoma SUFIAN MAFOTO BLOG
0 comments:
Post a Comment