Monday, January 20, 2014

AJALI YA NOHA YAUA 13 SINGIDA LEO

HABARI zilizotufikia hivi punde kutoka Singida zinasema watu 13 wamefariki dunia baada ya kutokea ajali ya magari mawili kugongana uso kwa uso eneo la Isuna mkoani humo.

Habari hiuzo zinasema ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Toyota Noah na lori ambayo namba zake za usajili hazikupatikana mara moja. Watu 13 waliofariki walikuwa katika Noah iliyokuwa ikitokea Itigi na maiti zao zimehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida.
Dk. Banuba aliwataja waliofariki kuwa ni Haji Mohammed (29) mkazi wa Msisi katika halmashauri ya Wilaya Singida, Salma Omari (mama), Omari Shabani (44) waliofariki pamoja na mwanao Nyamumwi Omari (10) wote wakazi wa Itigi wilayani Manyoni.

Wengine ni Ramadhani Mkanga, Mtuku Rashidi (68) na Salehe Hamisi (28), wote wakazi Sanjaranda Itigi wilayani Manyoni, Samir Shabani mkazi wa Puma, Mwaleki Nkuwi mkazi wa Ikungi (wote wakazi wa wilaya Ikungi) na Athumani Kalemba ambaye hajajulikana makazi yake.

Hata hivyo kamanda Kamwela pamoja na kuwataka madereva kuwa makini kipindi hiki cha masika pia alisema taarifa zaidi kuhusiana na tukio hili atalitolea ufafanuzi baada ya kukamilika upelelezi ikiwa ni pamoja na kumpata dereva na utingo wa lori ambao wamekimbia baada ya ajali.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu