picha akisindikizwa na askari polisi wa mahakama ya kisutu leo
MSANII wa Muziki wa Kizazi Kipya (bongo
fleva), Rashidi Abdallah Makwaro (29),maarufa kama Chid Benz, amefikishwa
mahakamani akikabiliwa na mashitaka matatu ikiwemo kukutwa na Dawa za kulevya
aina ya Heroin yenye thamani ya Sh. 38,638, bangi ya Sh. 1,720 na vifaa ya
kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.
Chid Benz amefikishwa mapema leo saa
3:00 asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa
ajili ya kusomewa mashitaka yake. Saa 7:50 mchana alifikishwa mbele ya Hakimu
Mkazi Mkuu, Warialwande Lema aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo.
Hata hivyo, hakimu aliamuru msanii huyo
kutolewa nje ili akave vizuri nguo baada ya suruali aliyokuwa amevaa mlegezo
maarufu kama kata kei kuonyesha nguo yake ya ndani.
“Kwanza mtoeni nje aende akavae nguo
hizo zinazodondoka…” aliamuru Hakimu.
Saa 7:54 alirejeshwa ndani ya chumba
cha mahakama upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwanaamina
Kombakono akisaidiana na Inspekta Jackson Chidunda, ulimsomea mashitaka
yake.Wakili Kombakono alidai kuwa Oktoba 24, mwaka huu katika uwanja wa Ndege
wa Julius Nyerere, uliopo Ilala jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alikutwa dawa
za kulevya aina ya heroin isivyo halali zenye uzito wa gramu 0.85.Katika
shitaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza, mshtakiwa
alikutwa na gramu 1.72 za bangi isivyo halali.Wakili huyo wa serikali alidai
kuwa, siku na eneo la tukio la kwanza na la pili, mshtakiwa alikutwa akiwa na
vifaa vinavyotumika kuvua dawa za kulevya aina ya heroin, kigae na kijiko huku
akijua ni kosa.
Mshtakiwa alikana mashitaka yote na
upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi na dhamana dhidi ya mshtakiwa.
Hakimu Lema alisema mshtakiwa atakuwa
nje kwa dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wanaotoka kwenye
taasisi zinazoamini na siyo walimu na dhamana ya Sh. Milioni moja.
Hata hivyo, mshtakiwa alishindwa
kutimiza masharti hayo na amepelekwa mahabusu hadi Novemba 11, kesi hiyo
itakapotajwa.
Chanzo;michuzi blog
|
0 comments:
Post a Comment