Afisa
habari wa Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akitoa mada kuu
iliyokuwa inahusu malengo ya maendelea ya milenia na kuangalia imefikia
wapi kwenye malengo hayo pamoja na kuwaelimisha kuhusu maendeleo
endelevu baada ya mwaka 2015(Post 2015 Sustainable Development)
iliyotolewa kwa Mtandao wa vijana wa Temeke.
Kituo
cha habari cha Umoja wa Mataifa jana iliandaa Alhamisi ya Burudani kwa
ajili ya kujifunza kazi mbalimbali za Umoja wa Mataifa. Kwa kila Alhamis
ya mwisho wa mwezi Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa huandaa
burudani kwa makundi mbalimbali na kujifunza kazi mbalimbali za Umoja wa
Mataifa. Alhamisi ya mwezi wa kumi kituo cha Habari cha Umoja wa
Mataifa kilitembelea Mtandao wa Vijana wa temeke na kujadili mambo makuu
ya malengo ya Milenia pamoja na kuangalia ni jinsi gani vijana
wanashiriki katika shughuri za kimaendeleo katika jamii zao
Mkutubi
- Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, Harriet Macha akisisitiza
jambo kwenye mada kuu iliyokuwa inahusu malengo ya maendelea ya milenia
na kuangalia imefikia wapi kwenye malengo hayo pamoja na kuwaelimisha
kuhusu maendeleo endelevubaada ya mwaka 2015(Post 2015 Sustainable
Development)
Mwenyekiti
wa Kituo cha Vijana wa Makangalawe, Ismael Mnikite akizungumza
jambo kuhusu mada husika na kuangalia ni njia gani zinaweza kuwapelekea
vijana kushiriki kwenye shughuli nzima za maendeleo
Mwenyekiti
wa Kituo cha Vijana wa Makangalawe, Ismael Mnikite akigawa
vipeperushi vya Umoja wa mataifa pamoja na fomu kwa vijana hao wa
Temeke.
Mada ikiendelea
Katibu wa Mtandao wa Vijana Temeke, Yusuph Kutengwa akichangia mada
Omari A. Mketo akichangia
Ishengoma
ambaye ni mlemavu wa macho akieleza faida alizozipata baada ya kituo
cha habari cha Umoja wa Mataifa kutoa mafunzo hayo kwa mtandao wa vijana
wa Temeke.
Baadhi
ya vijana wa mtandao wa vijana wa Temeke wakisoma kwa umakini malengo
ya milenia wakati kituo cha habari cha umoja wa mataifa walipokuwa
wanatoa mada kwa vijana hao
Picha ya pamoja
0 comments:
Post a Comment