Saturday, November 29, 2014

MATUKIO KATIKA PICHA AJALI YA CHOPA HUKO KIPUNGUNI DAR

 Helkopta aina ya Chopa iliyoanguka maeneo ya Kipunguni B Ukonga jijini Dar es Salaam, leo asubuhi na kuua watu wanne waliokuwemo akiwa ni rubani pamoja na askari watatu.
 Miili ya watu waliokuwemo kwenye helkopta hiyo ikiwa imekandamizwa na mabaki ya chopa hiyo.
 Sehemu ya mashuhuda wa maeneo hayo wakishuhudia ajali hiyo.
Helkopta inayosemekana inamilikiwa na TANAPA imeanguka na kuteketea kwa moto katika eneo la Kipunguni B Ukonga jijini Dar es Salaam leo asubuhi. 
Kwa mujibu wa mashuhuda, wamesema waliona helkopta hiyo ikipoteza uelekeo na badaye kuanguka chini hali iliyosababisha kishindo kikubwa baada ya kulipuka moto. 
Inasemekana ndani ya helkopta hiyo kulikuwa na watu wanne ambao wote wameripotiwa kufariki dunia.
Aidha imeelezwa kuwa katika ajali hiyo kulikuwamo na Askari 3 na rubani

*HELKOPTA YAANGUKA KIPUNGUNI DAR NA KUWAKA MOTO, YAUA

 Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Helkopta inayosemekana kuwa inamilikiwa na Tanapa imeanguka huko maeneo ya Kipunguni, na kuuwa watu wote wanne waliokuwa wakisafiri na helkopta hiyo.
Mashuhuda wakiwa eneo la tukio.

Helkopta inayosemekana inamilikiwa na TANAPA imeanguka na kuteketea kwa moto katika eneo la Kipunguni B Ukonga jijini Dar es Salaam leo asubuhi. 
Kwa mujibu wa mashuhuda, wamesema waliona helkopta hiyo ikipoteza uelekeo na badaye kuanguka chini hali iliyosababisha kishindo kikubwa baada ya kulipuka moto. 
Inasemekana ndani ya helkopta hiyo kulikuwa na watu wanne ambao wote wameripotiwa kufariki dunia.
Aidha imeelezwa kuwa katika ajali hiyo kulikuwamo na Askari 3 na rubani Blog sufian mafoto
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu