Thursday, December 18, 2014

MTANZANIA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KUUA WATOTO WAKE

Charles Mihayo akishikiliwa na polisi

MTANZANIA anayeishi nchini Austaralia, Charles Mihayo ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya kuwaua kikatili watoto wake mwenyewe ili kumkomoa mkewe aliyekuwa ameachana naye amehukumiwa kifungo cha maisha jela.
Mihayo mwenye miaka 36, alifanya ukatili huo kwa wanae Savannah (4) na Indianna (3) Aprili 20, 2014 nyumbani kwake huko Melbourne na amehukumiwa leo kifungo hicho.
Inadaiwa kuwa baada ya kuachwa na mke wake, hasira zilimfanya bwana Mihayo kuamua kufanya ukatili wa kukatisha uhai wa watoto wake mwenyewe Savannah (4) na Indianna (3), ili tu kumuumiza mke wake kama njia ya kumlipizia kisasi. Inadaiwa kuwa aliwauwa kwa kuwakandamiza na mto baada ya kucheza nao.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa siku mauaji hayo yalipofanyika, mama wa watoto hao aliwapeleka kwa baba yao bwana Mihayo. Baada ya kuwafikisha baba yao aliwafanyia shopping ya nguo na viatu vipya.
Kabla ya kutenda ukatili huo kwa damu yake mwenyewe, Mihayo aliwarekodi video wakicheza muziki huku akicheza nao. Na katika video ambayo polisi baadae waliiona, alisikika akiwaambia binti zake wamuoneshe mama yao nguo mpya alizowanunulia, na walifanya hivyo na kisha mwanaume huyo akakaa mbele ya camera na kusema “tutamuonesha mama kitu kingine dakika kumi zijazo”, na kuendelea kucheza nao hadi alipowakandamiza na mto (pillow) hadi kufa.
Baada ya kufanya mauaji Mihayo mwenyewe aliwapigia simu polisi ambao baada ya kufika nyumbani kwake wakiwa mlangoni aliwaambia , “Tayari, nimewaua. Nimewaua watoto wangu. Inabidi mumuulize huyu [mama yao] sababu.”
Polisi waliwakuta watoto hao wakiwa tayari wamefariki huku wakiwa wamevalishwa nguo na viatu vipya ambavyo walinunuliwa na baba yao siku hiyo.
Licha ya kuhukumiwa kifungo cha maisha, Charles Mihayo anatakiwa kutumikia kifungo cha miaka 31 kabla ya kupata haki ya kupewa msamaha.

Savannah (4) kulia na Indianna (3) kushoto

Savannah (4)kulia  na Indianna (3) 



Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu