2

SI LA KULIKOSA

Tuesday, June 2, 2015

BREAKING NYUZZZZZ......: MBUNGE WA UKONGA, MH. EUGENE MWAIPOSA AFARIKI DUNIA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA

TANZIA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam, Mhe. EUGEN ELISHIRINGA  MWAIPOSA  kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 2 June 2015 nyumbani kwake Dodoma ambako amekuwepo kushiriki Mkutano wa Bunge la Bajeti.
Mwili wa Marehemu utaagwa kesho tarehe 3 Juni 2015 kuanzia saa 4 asubuhi katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, na baadaye mwili kupelekwa nyumbani kwake Ukonga, Dar es Salaam.
BWANA alitoa, BWANA ametwaa. Jina la BWANA  lihimidiwe. Amina!
Imetolewa na Ofisi ya Bunge,
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa,
Dodoma,
Wabunge wakiangua vilio a bunge mara baada ya kutangazwa kifo cha mbunge huyoMwaiposa (kushoto) enzi za uhai wake, akiteta jambo na Mkuu wa Polisi wilaya ya Kipolisi Stakishari, OCD Julio Simba 

Marehemu Mwaiposa, (kulia), akiwasikiliza waliokuwa wapiga kura wake

Marehemu Mwaiposa, (kulia), akisalimiana na waziri mkuu, Mizengo Pinda, wakati wa uhai wake. Katikati, ni mbunge wa viti maalum, AL-Shymaa
2 Juni 2015.  
MBUNGE WA UKONGA, MWAIPOSA AFARIKI DUNIA Mama Eugene Mwaiposa enzi za uhai wake Mbunge wa Ukonga Eugene Mwaiposa kafariki majira ya saa nne asubuhi mjini Dodoma. Haijafahamika vema kama alikuwa anaumwa nini, lakini taarifa za awali zinasema, Amefia Rock hotel, jirani na kituo cha mafuta cha Shabiby. TAARIFA YA NAIBU SPIKA Bunge la jamhuri limepata msiba wa kufiwa na mbunge wa jimbo la Ukonga, alikuwa na tatizo la shinikizo la damu kwa muda mrefu, Amefariki nyumbani kwake hapa Dodoma. Nyumbani kwa marehemu ni eneo la Chaduru opposite na jengo jipya la hoteli ya Shabiby barabara ya Dar es Salaam, Mwili umepelekwa hospitali ya mkoa wa Dodoma kwa uchunguzi zaidi. Shughuli ya Kuaga itafanyika kesho baada ya familia yake kuwasili hapa Dodoma. Tutatumia mtandao wa simu kuwajulisha taarifa zaidi, kwa jinsi hio natumia kanuni ya 152 kuahirisha bunge hadi keshokutwa Alhamis.Bonyeza HAPA kusikiliza sauti.

Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu