Thursday, July 30, 2015

BREKING NEWZZZZ LOWASSA ALAKIWA NA MAELFU APIGA PEOPLEEES..POWER

Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa akiwa sambamba na Mkewe Mama Reginal akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam
 
 
 WAZIRI Mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa, (kulia), akionyesha mkoba wenye fomu za kuomba kuwania urais kupitia CHADEMA, baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Mh. Freeman Mbowe, kwenye makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo Julai 30, 2015. Mh Lowassa, alijiunga hivi karibuni na chama hicho, baada ya kujitoa CCM
 Mh. Lowassa, akipokea mkoba wenye fomu hizo kutoka kwa Mwenyekiti Mbowe, huku Mama Regina Lowassa, mke wa Mh. Lowassa, akishuhudia

 Mh. Lowassa, akiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu, na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, (Zanzibar), Salum Mwalimu
 Baadhi ya wafuasi wa CHADEMA, wakionyesha kadi za kupigia kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2015, wakati wakisubiri kumuona Mh. Lowassa, makao makuu ya CHADEMA jijini Dar es Salaam Julai 30, 2015
 Mh. Lowassa, akiongozana na Mkewe, wakati akiwasili makao makuu ya CHADEMA, Kinondoni jijini Dar es Salaam Julai 30, 2015
 Mh. Lowassa, akiwapungia mkono wafuasio wa CHADEMA, wakati akiondoka makao makuu ya chama hicho, baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na chama hicho kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015
 Mh. Lowassa, akitoa hotuba baada ya kuchukua fomu
 Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, akihutubia kwenye hafla hiyo
 Mh. Lowassa, "akipiga" People's..................Power


Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa pichani akiwapungia wanachama na wafuasi mbalimbali wa chama cha CHADEMA waliofika kumshuhudia akiwa sambamba na Mkewe Mama Regina akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam.






 WAZIRI MKUU MSTAFF EDWARD LOWASSA KATIKA SAFARI MATGEGEMEO  AKILAKIWA CHADEMA LEO
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu