NA K-VIS MEDIA NA
Mashirika ya Habari
IKIWA ni siku nne
tangu msichana wa Kitanzania mwenye miaka 20 anayesoma mjini Bangalore nchini
India, kudhalilishwa kwa kuvuliwa nguo na kutembezwa uchi, imeripotiwa Polisi
kuwa waliamuriwa na polisi mjini humo kuzima simu zao, Kiongozi wa Wanafunzi
Waafrikawanaosoma mjini humo, Bosco Kaweesi amesema.
Kiongozi huyo ambaye
pia ni mshauri wa kisgeria wa wanafunzi, ameliambia Jarida la kimtandao
Hindustan Time (HT), kuwa polisi walikuwa wanajaribu kuwabana wanafunzi hao ili
ukweli na habari kuhusu tukio hilo zisisambae.
Msichana huyo
aliyekuwa akisafiri na rafiki zake wengine watatu wa kiume, kwenye garidogo,
alikumbana namkasa huo, baada ya kufikaeneo la tukio la ajali iliyosababishwa na
raia mmoja wa Sudanaliyemgonga mtu na mkewe na kusababisha kifo cha
mwanamke.
Baada ya muda kidogo
ndipo Mtanzania huyo na wenzake w
akipita kwenye eneo hilo, walisimamishwa na kuchomolewakutoka ndani ya gari
hilo, ambapo wavulana hao walikimbia na kumuacha msichana huyo mikononi mwa
genge hilo la watu ambao walimvua nguo na kumtembeza mitaani ikiwa ni pamoja na
kumpiga.
Tukio hilo
limetafsiriwa na Dunia kuwa ni ubaguzi wa rangi, madai ambayoSerikali ya India
pamoja na polisi wamekanusha kuhusisha tukio hilona ubaguzi wa
rangi.
Kiongozi wa chama cha
wanafunzi wa Tanzania walioko mjini humo, aliyetambuliwa kwa jina moja la Helen,
amewalaumu polisi kwa kujaribu kuficha ukweli.
Tayari Waziri wa
Mmambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda, Afrika Mashariki na Kimataifa, Balozi
Dkt. Augustine Mahiga, ameliambia Bunge kuwa Serikali inalifuatilia suala hilo
kwa karibu sana, na tayari wameambiwa na Serikali ya India kuwa watu watatu
wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment