Thursday, February 18, 2016

PAMBANO LA WATANI WA JADI YANGA NA SIMBA

Kesho jumamosi   ni siku ya pambano la jadi katika mchezo wa soka  wa ligi kuu ya vodacom kati ya YANGA NA SIMBA  Timu hizi ni kongwe katika mchezo wa kabumbu hapa  zinapocheza basi huwa mioyo ya washabiki wa pamde zote  viroho vinawadunda  kwanza mchezo wenyewe hautabiriki
 lakini ngoja niwakumbushe  kidogo mashabiki wa klabu ya Simba  Sports club  timu hoyo ya wekundu wa msimbazi  ilikuwa inafahamika  kama Sundarland  Sports Club (SSC) kama ilivyo timu ya uingereza  lakini rangi ya jezi ni hiyo hiyo nyekundu na nyeupe  haijabadilika mpaka leo  dam na wakati huo ilikuwa makao makuu ya klabu hiyo ni makutano ya barabara ya kongo na mchikici hivi sasa kuna jemgo la HH Amoni , rai wa jamhuri ya muungano wakati huo ni Hayati mwalim Nyerere

Alisema sasa kunahaja ya kutumia majina ya asili  kwa kila mtu badala ya kutaja majina mawili kwa mfano juma omar na badala yake watumie majina na ya ukoo ili kurahisisha na pia vilabu vya mipira nao wasitumie majina ya kigeni  ndipo  vilabu vungi vikanza kutafuta majina ya kizalendo  ndipo katika kufikiri sana ili wasipoteze  maana ya herufi za SSC  wakaamua  kujiita  SIMBA SPORTS CLUB hata timu ya Ashanti  ilikuwa inaitwa Liverpool ,hata Cosmo  ilikuwa inaitwa Cosmopolitan


YANGA Timu ya Yanga imeanza miaka mingi huku washabiki wengi wanaifahamu timu hiyo maskani yao yako mtaa wa Jangwana na Twiga  timu ya yanga inapokutana na watani zao Huwa mshike mshike  na nguo huchanika  klabu ya yanga watu wengi wanafahamu pale ndio walipoanzia makao makuu yao yalianzi katika makutano ya mtaa wa Sukuma na Mafia jijini Dar es salaam Jina kamili Youngs Africans maana yake vijana wa kiafrika  lipotoka hapo walihamia katika makutano ya mtaa wa Mafia na Nyamwezi  si mbali sana na walipokuwa awali   katika klabu mbili hizi maarufu katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki  hususani Tanzania wanachama wa klabu hizi nyakati hizo linapotangazwa  pambano la watani wa jadi kuchezo mwezi fulani basi ikiwa imebaki wiki moja

katika vijiwe vya washabiki na wanachama u7yakuta unachoma ubani kinawekwa chungu huku wakichomeka bendera za vilabu vyao Simba na Yanga  wanakesha kila kona katika jiji la Dar es salaam na mikoani lazima utakuta ubani  unachomwa   huku

Mashabiki wa klabu hizo wanapokwenda uwanjani  wanakuwa na Bendera zao kuuuubwa Shabiki wa yanga wakati mpira hauja anza  wanashika bendera zao wanazunguka uwanjani wakitambiana  hivi wanakwenda na wakati nilikuwa nawakumbushia pambano la jadi linavyokuwa hivi sasa ni kuvaa jezi tu na matarumbeta   angali mzuka tunakujuza zaid  wakati huo timu hizi zilivyokuwa zinapeana majina ya utani na mengine hujiita wenyewe

ANGALIA MZUKA NA KUPATA HABARI ZAIDI





Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu