Kikosi
cha Uchukuzi SC kilichotinga nusu fainali ya soka ya mashindanoya Mei Mosi
yanayoendelea kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Kikosi
cha Tamisemi kilichoingia nusu fainali katika michezo ya Mei Mosi.
Kipa wa GGM Emmanuel Charles (mwenye jezi nyeusi) akijiandaa kudaka mpira
wa kona uliochongwa na Omar Said ‘Chidi’ wa Uchukuzi (hayupo pichani). Timu
hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
Na
Mwandishi Wetu, Dodoma
TIMU
nne za soka zimeingia hatua ya nusu fainali kwenye mashindano ya Mei Mosi yanayoendelea
kwenye atika uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.
Timu
hizo ni Tamisemi na Tanesco zilizotoka kundi A, wakati za kundi B ni Uchukuzi
SC na Geita Gold Mine (GGM).
Nusu
fainali hiyo itafanyika keshokutwa kwa kumshindanisha mshindi wa kwanza wa
kundi A na mshindi wa pili wa kundi B kwa mechi ya saa 8:00 mchana na mechi ya
saa 10:00 mshindi wa kundi B ataumana na mshindi wa pili wa kundi A.
Timu
zilizoishia kwenye hatua ya makundi ni TPDC, CWT na UDOM za kundi A na za kundi
B ni Ukaguzi, CDA na Mambo ya Ndani.
Kwa
upande wa netiboli inayochezwa kwa mtindo wa ligi, timu ya Tamisemi inaongoza kwa kuwa na pointi
sita sawa na Uchukuzi SC, lakini wanamagoli mengi ya kufunga ambayo ni 76
wakati wenzao wanayo 54, wakifuatiwa na CDA yenye pointi tatu, huku Tanesco na
TPDC wakiwa hawana kitu.
Katika
michezo ya awali ya kuvuta kamba timu ya wanawake ya Uchukuzi SC ilipata
ushindi wa chee dhidi ya UDOM, ambao hawakutokea uwanjani, pia Tanesco wanaume
walipewa pointi baada ya CWT kushindwa kuonekana ulingoni, nayo TPDC wanawake
waliwavuta Tamisemi kwa mivuto 2-0.
Katika
mchezo wa bao wanawake Mayasa Kambi wa UDOM alitwaa ubingwa akifuatiwa na Thea
Samjela wa Uchukuzi SC na mshindi wa tatu ni Catherine Likunguwa wa CDA; wakati
kwa wanaume Omari Said wa Uchukuzi SC alitwaa ubingwa baada ya kumfunga Lameck
Mboje wa Tamisemi katika mchezo wa fainali.
Nayo
TPDC ilitoshana nguvu na Tanesco katika soka kwa kufungana bao 1-1. Tanesco
ndio walikuwa wa kwanza kufunga bao katika dakika 25 na TPDC walisawazisha
katika dakika za nyongeza.
Michuano
hiyo itaendelea Jumanne (Aprili 26,2016) katika soka kwa Uchukuzi SC
kuwakaribisha CDA Dodoma asubuhi na jioni Ukaguzi watacheza na Mambo ya Ndani.
0 comments:
Post a Comment