Thursday, April 21, 2016

WAKATI wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika,  (CAF Champions league), Yanga ikitolewa na El-Ahly National ya Misri kwa jumla ya mabao 3-2 usiku wa kuamkia leo Aprili 21, 2016, polisi mjini Alexandria, walilazimika kurusha mabomu ya machozi kusambaza washabiki wa timu hiyo kongwe ya waarabu.
Polisi walichukua uamuzi huo kuwatawanya maelfu ay washabiki wa El-Ahli waliotaka kuingia kwenye uwanja wa Borg El-Arab mjini Alexandria, ambapo Yanga ilikuwa ikimenyana na El-Ahli kwenye mchezo wa marudiano raundi ya 16 ya michuano hiyo ambapo katika pambano hilo, Yanga ilifungwa mabao 2-1 na hivyo kutolewa kwenye michuano hiyo kwa jumla ya mabao 3-2 ikizingatiwa kwenye mchezo wa awali uliochezwa jijini Dar es Salaam wiki moja iliyopita, timu hizo zilitoka are ya bao 1-1 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
ATaarifa ya polisi mjini Alexandria ilisema “Tulijaribu kuwashawishi waondoke, lakini walipinga na kujaribu kuingia uwanjani kwa nguvu ambapo polisi wa kutuliza ghasia walilazimika kufyatua mabomu ya machozi ili kuwatawanya” taarifa hiyo ilisema.

Watu 29 walipoteza fahamu kwenye ghasia hiyo
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu