Wednesday, May 18, 2016

KITUO CHA KISASA TIBA ASILI MIZANI HERBAL


 Mkurugenzi Mtendaji na Tabibu mkuu wa Mizani Herbal and Natural Therapies, Bw. Abalhassan Jumar(kulia), akiwa na wasaidizi wake kwenye kliniki hiyo mpya ya tiba asili iliyoko Sinza-Palestina jijini Dar es Salaam.
 NA K-VIS MEDIA
KITUO kipya na cha kisasa cha tiba asili, MIZANI herbal and Natural Therapies kimefunguliwa Sinza Palestina jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na K-VIS MEDIA jijini Dar es Salaam, Mei 10, 2016, Mkurugenzi  Mtendaji wa kituo hicho Bw. Abalhassan Jumar, amesema kuwa, kliniki yake  inaendesha tiba  asili kwa kutumia sawa zitokanazo na mimea na matunda na kwamba wanatoa matibabu ya aina mbalimbali.

Alitaja baadhi ya magonjwa yanayotibiwa kwenye kituo hicho  ni pamoja na maumivu ya tumbo, kichwa, ganzi katika mwili, kuwashwa mwili, michirizi ya mishipa ya damu katika mwili hususan akina mama, upungufu wa nguvu za mwili na kuongeza hisia mbalimbali katika mwili, tiba  bora ya matatizo ya uzazi kwa mlengwa.
"Pamoja na kutoa tiba kwa kutumia dawa zitokanazo na mimea na matunda lakini pia tunatoa ushauri kwa wale wenye matatizo mbalimbali mwilini." Alisema Bw.Abalhasan.
Katika kuhakikisha wagonjwa wanaofika kwenye kituo hicho wanapata huduma katika mazingira bora na ya kisasa, kituo kina ukumbi wa kupumzika watu wanaofika kupata huduma ambapo ofisi  zina viyoyozi na huduma nyingine. Alisema Abalhassan ambaye pia ndiye tabibu mkuu.
Akifafanua zaidi mkurugenzi huyo wa Mizani Herbal and Natural Therapies Ltd alisema, katika kuonyesha mgonjwa anasikilizwa zaidi maelezo yake, ubora na uimarikàji wa afya ya muhusika yatazingatiwa kwanza  kabla mtaalamu wa Mizani  hajaanza kutoa maelezo  yake. Alifafanua Mkurugenzi  huyo.

 Dawa zitokanazo na mines zikiwa kwenye vifungashio

 Tabibu mkuu, Abalhassan akiwa ofisini kwake.

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu