Saturday, June 4, 2016

 Nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta, akimtoka mchezaji wa timu ya taifa ya Misri, Tarek Hamad Hemed, katika pambano la soka la marudiano la michuano ya kufuzu kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika, 2017 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam leo Juni 4, 2016. Taifa Stars ambayo ilikosa penalti, ilinyukwa mabao 2-0 na hivyo kuondoa matumaini ya kuweza kufuzu kucheza fainali hizo. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)








 Shabiki wa Taifa Stars, akiwa na uso wa huzuni baada ya timu hiyo kunyukwa mabao 2-0 na timu ya Taifa ya Misri kwenye pambano la marudiano la michuano ya kufuzu kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo Juni 4, 2016. Pamoja na kipigo hicho, nahodha wa timu hiyo Mbwana Samatta, alikosa penalti na hivyo kuzidisha huzuni kwa atanzania.(Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)






 Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa, akionyesha huzuni wakati timu yake ikiwa nyuma kwa mabao 2-0 dhidi ya timu ya taifa ya Misri kwenye mchezo wa marudiano wa michuano ya mchujo ya kuwania kucheza fainaki za kombe la mataifa ya Afrika (African Cup of Nations 2017-Qualifiers), kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo Juni 4, 2016. Taifa Stars ilikosa penalti, iliyopigwa na nahodha wa timu hiyo Mbwana Samatta. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
 Bao la kwanza la Misri lililofungwa kwa njia ya mkwaju wa adhamu ya moja kwa moja (Free Kick)
 Nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta, (kulia), akikokota mpira mbele ya mchezaji anayecheza ligi kuu ya Uingereza kwenye klabu ya Arsenal, Mohammed Nasser Elsayed
 Mkwasa akiwaelekeza vijana wake
Mashabiki wa Taifa Stars, wakiwa na nyuso za kuhamanika
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu