.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya
kuhudumia mizigo, Ndege na abiria ya Swissport inayotoa huduma katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), alipofanya ziara ya siku moja ya kutembelea uwanja huo Dar es Salaam leo.
Kamanda wa Polisi wa Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Kamishna Msaidizi (SACP), Martin
Otieno (kulia), akimueleza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Profesa Makame Mbarawa (kushoto), kuhusu hali ya usalama katika uwanja
huo wakati wa ziara ya waziri huyo katika uwanja huo Dar es Salaam leo.
(Katikati) ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), Mhandisi George Sambali,
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Swissport, Gaudence Temu (wa pili kushoto), akimuelekeza Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili
kulia), jinsi kampuni hiyo inavyofanyakazi na changamoto zake. Kulia ni Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi George
Sambali. Kushoto ni Meneja Biashara wa TAA, Efata Lyimo.
Vifufushi vikiwa kwenye ghara jipya la Swissport.
Foku lifti likifanya kazi ya kubeba mizigo katika ghara hilo.
Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji, Elizabeth
Lukuwi (kushoto), akutoa maelezo kwa Waziri Mbarawa baada ya kufika
eneo la ukaguzi kwa wageni.
Kamishna Msaidizi wa
Uhamiaji, Elizabeth Lukuwi, akimpigia saluti Waziri Mbarawa baada ya
kumpa maelekezo ya utendaji kazi katika kitengo cha wageni kiwanjani
hapo.
Waziri Mbarawa akizungumza na Raia wa
Kigeni aliyemuelezea kutumia muda mwingi zaidi ya masaa mawili kwa ajili
ya upimaji wa afya uwanjani hapo ambapo Waziri huyo aliwaagiza wahusika
kuhakikisha wanatumia muda mfupi kutoa huduma kwa wageni ambao wanakuwa
wamerundikana katika eneo hilo.
Baadhi ya wafanyakazi wa JNIA wakiwa uwanjani hapo.
Ofisa Usalama wa Kampuni ya Ujenzi ya
Kimataifa ya Bam, Zueri Salum Mbungu akitoa maelezo kwa waziri Mbarawa
(hayupo pichani) na ujumbe aliongozana nao kuhusu hatua za usalama
kabla ya kwenda kukagua ujenzi wa mradi wa Uwanja wa ndege wa Terminal 3
unaojengwa na kampuni hiyo.
Taswira ya jengo la mradi wa Terminal 3 unavyoonekana katika hatua ya ujenzi.
Waziri Mbarawa (katikati) na ujumbe wake wakiendelea na ukaguzi wa Mradi wa Terminal 3.
Meneja Biashara wa Kampuni ya Ujenzi ya
Kimataifa ya BAM inayojenga Mradi wa Terminal 3, Chris Bowers (kulia),
akimuelekeza jambo kuhusu ujenzi wa uwanja huo.
Taswira ya timu nzima iliyoongoza na Waziri Mbarawa wakati wa kutembelea uwanja huo.
0 comments:
Post a Comment