Friday, July 22, 2016

Meneja Program wa SATF Rogasian Massue, (kulia), akipeana mikono na meya wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob, wakati akikabidhi madawati hayo

NA JANET JOSIAH.
MSTAHIKI Meya wa Halimashauri ya Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob Leo Julai 22, 2016, amepokea msaada wa madawati 100 toka Shirika la Social Action Trust Fund (SATF)lenye makazi yake Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo fupi Meya Jacob alisema kwamba mpango ulipo kwa Manispaa hiyo nikuhakikisha hadi mwezi Agosti mwaka huu, hakuna mwanafunzi atakayekaa chini kutokana na kuwa na uwezo wa kuwatosheleza.
" Nawashukuru sana nyie Shirika la SATF kwa msaada wenu huu kwetu Manispaa... tunawaalika wadau wengine wa elimu kutuletea msaada mwingine wa madawati ili yajae na mengine tuweke stoo akiba ili watoto watakapovunja wapewe mengine maana ni watundu sana" alisema
Pamoja na hilo Meya Jacob   aliwataka wadau wengine wa elimu kujitokeza kutoa msaada wa madawati kwa kuwa uhitaji wake bado upo.
Hata hivyo alisema kuwa mpaka sasa wazabuni waliopewa kazi ya kutengeneza madawati zaidi ya 16000 wanaendelea ili yaanze kugawiwa kwa shule za Manispaa hiyo haraka.
Mapema Meneja Program wa SATF Rogasian Massue alisema kuwa watoa madawati yao 100 kama mpango wao wa kusaidia wilaya mbalimbali ili vijana waweze kupata elimu na kuwa wataalam mbalimbali.
Massue alisema katika program ya kutoa msaada wa madawati 150 katika  Halmashauri ya Chato mkoani Geita, wakafuatilia Kinondoni jijini Dar es Salaam madawati 100.
Meneja program huyo alisema sasa wanajiandaa kupeleka msaada Manispaa za Temeke na Ilala za hapa jijini, wilaya ya Kankonko mkoani Kigoma na  Kaliua  mkoani Tabora.


 Meya Jacob
Meneja Program wa SATF Rogasian Massue, (kushoto), akizungumza wakati wa makabidhiano hayo
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu