(Picha na Sultani Kipingo)
|
Na
Sultani Kipingo
Mfalme
wa Afro Pop nchini Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent)
anavunja ukimya na kurejea kwa kishindo kwenye anga ya muziki, huku akiwa msanii wa kwanza kusaini mkataba
na lebo mpya ya KOMBINENGA inayoendeshwa na producer nguli John Shariza a.k.a
Mann Water.
Twenty
Percent, ambaye mwaka 2011 alitwaa tuzo saba za Kilimanjaro Music Awards (KTMA)
kwa mpigo, huku Mann Water akisomba tuzo mara mbili mfululizo za producer bora (mwaka 2013 na 2014), tayari
amesharekodi vibao vitano na anatarajia kuachia ngoma moja mpya ya kwanza Julai
18, 2016, katika kuandaa albamu yake ya SAUTI YA GHARAMA.
"Nimerudi
kuwachinja tena" anasema Twenty Per cent, akiwa anakamilisha kurekodi
katika studio za Combination Sounds iliyoko Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es
salaam. "Nimerudi kurudisha sauti ya gharama kwa jamii. Sauti inayofundisha. Sauti inayoonya.
Sauti inayoburudisha. Sauti inayozengua kila mtu, " anaogeza.
Tayari
Tweny Per cent ameshasaini mkataba wa miaka mitano na lebo ya KOMBINENGA,
katika hafla fupi iliyofanyika Jumapili katika ofisi za Combination Sounds.
Kuanzia sasa shughuli zote za msanii huyu zitasimamiwa na lebo hiyo chini ya
Producer Mann Water.
Wakili
msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys ndiye aliyefanikisha zoezi hilo la
kutiliana saini mkataba lililoshuhudiwa pia na meneja uzalishaji wa Combination
Sounds, Rowel Moses.
"Namkubali
sana
Twenye Pa kwani ni msanii aliyetimia na hutumii shuruba wakati wa
kurekodi
maana ana kipaji cha ajabu cha kutunga akiwa wima na kukariri hapohapo",
anasema Mann Water, ambaye ameshafanya kazi na wasanii nyota kibao
wakiwemo Lady Jay Dee, Ali Kiba, Ommy Dimpoz, Christian Bella, MB
Dogg, Juma Nature, Mr Blue na wengine wengi.
Twenty
Percent alitamba sana tokea mwaka 2006 kwa wimbo wake wa "Manemane"
uliomfanya ashinde tuzo ya KTM, kabla ya kuweka historia ya kusomba tuzo saba
kwa mpigo mwaka 2011. wakati huo nyimbo zilizompandisha chati zilikuwa ni
"Tamaa Mbaya" na "Ya nini
Malumbano" na "Maisha ya Bongo"
Mbali na Muziki Twenye Percent pia alitamba sana kwenye tasnia
ya filamu ambapo alicheza kwenye mchezo uliofahamika kwa jina lake la 20%.
Baada ya hapo akaamua kupumzika kwa muda na kujishugulisha na shughuli za kilimo.
"Kilimo kinaendelea vyema na sasa nimeamua kurudi kwenye gemu ili
kuwachinja tena" alimalizia, akiinuka kuelekea kwake Kimzichana, Mkuranga,
Mkoa wa Pwani, anakoishi.
0 comments:
Post a Comment