Miss Tabata
kufanyika leo Da West Park
Na Mwandishi
Wetu
SHINDANO la
kumsaka mrembo wa kitongoji cha Tabata mwaka huu Miss Tabata 2016 linafanyika leo Ijumaa kwenye Ukumbi wa Da West Park, Tabata
jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa
shindano hilo Joseph Kapinga alisema jana kuwa jumla ya warembo 16 wanatarajia
kupanda jukwaani kuwania taji hilo linaloshikiliwa na Ambasia Mallya, ambaye
alishinda taji hilo mwaka 2014.
Mratibu huyo
aliwataja warembo watakaoshiriki kuwa ni pamoja na Happiness Paul (21), Neema Makwaia
(21), Rose Lucas (22), Mariam Maabadi 23), Sabrina Khalifa (20), Catherine Alex
(22) na Grace Malikita (21).
Warembo wengine
ni Rachel George (21), Nasra Munna (23), Jackline Evarest (21), Flora Msigwa
(21), Noela Pastory (21), Neema Zablon
(24) na Jesca Jackson (22).
Aliongeza
kuwa warembo watano watakaofanya vizuri katika shindano hilo, watapata tiketi
ya kuiwakilisha Tabata katika shindano la Kanda ya Ilala baadaye mwaka huu.
Alisema kuwa
warembo watakaoingia tano bora kila moja atazawadiwa kusoma nafasi ya kusoma kozi
yoyote katika Chuo cha DataStar Training College. Kila kozi itagharimu 1.8m/-
Mshindi wa
kwanza pia atapata fedha taslimu Sh. 300,000
wakati mshindi wa pili ataondoka na Sh. 200,000 huku mrembo atakayeshika nafasi
ya tatu atajinyakulia Sh. 150,000 . Mshindi wan ne na watano kila mmoja atapata
Sh. 100,000 huku kifuta jasho cha Sh. 50,000 kila m Wengine ni Rachel George
(21), Nasra Munna (23), Jackline Evarest (21), Flora Msigwa (21), Noela Pastory (21), Neema Zablon (24), Narcisa Wilbert (19) na Jesca Jackson (22).
moja
kitatolewa kwa waliobakia.
Bendi ya
Twanga Pepeta itatumbuiza kwenye shindano hilo linaloandaliwa na Keen Arts na
Bob Entertainment.
Nae
Mkurugenzi wa Miss Tabata ambae pia ni mkuu wa kambi Godfrey Kalinga alisema
jana kuwa maandalizi ya shindano limekamilika.
Miss Tabata
inadhaminiwa na Lete Raha, DataStar College, Global Publishers, CXC Africa,
Fredito Entertainment, Yono Auction Mart, Saluti5, Kitwe General Traders na Bob
Entertainment.
0 comments:
Post a Comment